Featured Kitaifa

SERIKALI YA DENMARK YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark, Mhe. Flemming Møller Mortensen pembezoni mwa Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika tarehe 14 Juni 2022 jijini Helsinki, Finland.
Mazungumzo baina ya Mawaziri hao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia pamoja na kuendeleza sekta za biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu na uchumi wa kijani.

Pia Waziri Mulamula ameishukuru Denmark kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo kabla na baada ya Tanzania kupata uhuru wake mwaka 1961 na kwamba Serikali ya Tanzania inaendelea kusimamia kwa karibu mipango na miradi yote iliyoanzishwa kwa ushirikiano na Serikali ya Denmark.

Waziri wa Maendeleo wa Denmark, Mhe. Flemming Møller Mortensen (wa pili kushoto) akieleza kuhusiana na maeneo ya kimkakati ambayo Serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuenzi ushirikiano wa kihistoria ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo mawili.

Waziri Mulamula akimkabidhi zawadi, Mhe. Mortensen

Ujumbe ulioambatana na Mhe. Balozi Mulamula ukifuatilia mazungumzo.

About the author

mzalendoeditor