Featured Kitaifa

MTINDO USIOFAA WA MAISHA UNACHANGIA ASILIMIA 80 YA MAGONJWA YASIAMBUKIA,VISA VIPYA 42000 SARATANI, WATU MILIONI 5 SHINIKIZO LA DAMU LA JUU KWA MWAKA

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi msaidizi anayeshughukia magojwa ya yasiyoambukiza kutoka wizara ya afya Dk.James Kiologwe  akiongea na waandishi wa habari katika mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari na wauguzi, yanayoendelea mkoani Arusha.
Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Sylivia Mamkwe akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha baada ya kufungua mafunzo ya madaktari na wauguzi yanatolewa na wizara ya Afya.
…………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Imeelezwa kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza mwaka hadi mwaka ambapo ndani ya mwaka mmoja kumekuwa na visa vipya vya Saratani elfu arobaini mbili kwa mwaka pamoja na watu milioni 5 kuwa na shinikizo la damu la juu huku asilimia 26 wakiwa ni  watu wazima.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi msaidizi anayeshughukia magojwa ya yasiyoambukiza kutoka wizara ya afya Dk.James Kiologwe katika mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari, wauguzi na waratibu juu ya magonjwa yasiyoambukiza ambapo alisema kuwa pia Kuna watu zaidi ya milioni 1wenye tatizo la kisukari.
Dkt Charles alifafanua kuwa watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa seli Mundo ni zaidi ya 11 kwa mwaka ambapo magonjwa hayo mengi yasiyoambukiza yanasababishwa na mitindo isiyofaa ya maisha hasa ulaji, matumizi ya vilevi kama vile pombe na tumbaku ambayo inachangia kwa zaidi ya asilimia 80.
“Jambo baya zaidi ni kwamba katika wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu zaidi ya asilimia 75 hawajijui kama wana tatizo hilo badala yake wanakuja kugundulika baada ya kwenda vituo vya afya kutokana na madhara ya shinikizo hilo kama vile kupata Kiharusi na matatizo mengine,” Alieleza.
“Lakini pia asilimia 64 ya wagonjwa wenye tatizo la sukari hawajijui ambapo na wao  wanagundulika baada ya kupata madhara kutokana na tatizo hilo  na hii inatokana na kutokuwepo kwa elimu katika jamii juu ya kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara,” Alifafanua.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Sylivia Mamkwe wakati akifua mafunzo hayo alisema mafunzo hayo  yatasaidia katika kuleta mapinduzi ya kutibu magonjwa yasiyoambukiza kwani kutokana na magonjwa hayo kunatokea vifo hivyo hawana budi kuwekeza zaidi katika huduma za afya za mwanzoni kwa kupeleka huduma chini.
Alisema watapeleka wataalamu wa magonjwa hayo kwenye vituo vya afya huku lengo lao likiwa ni hadi katika ngazi ya Zahanati kwasababu yamekuwa mzigo na kwa kuangalia katika kila familia hakosekani mtu mmoja mwenye magonjwa hayo.
“Mliopo hapa mmefundishwa naomba Sasa tukaone kazi zenu kwenye vituo vyenu vya kazi lakini pia huu umekuwa wakati muafaka wa serikali ambapo upo katika mpango mkakati wa kuzui  na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ambao ni wa 2021/2026 na itahisisha kuhakikisha watoa huduma wanapewa mafunzo,” Alisema Dkt Mamkwe.
Hata hivyo mafunzo hayo yamehusisha watumishi wa Afya 360 kutoka mikoa ya Arusha, Manyara na Singida na yatafanyika kwa siku tano.

About the author

mzalendoeditor