Featured Kitaifa

RC MALIMA AIPONGEZA REA KWA KAZI NZURI WANAYOFANYA

Written by mzalendoeditor
MKUU wa Mkoa
wa Tanga Adam Malima akizungumza na Bodi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Julius Kalolo wa Pili kulia na Watendaji wa
Wakala huo waliofika ofisini kwake kabla ya kuanzia ziara ya kuelekea Kijiji
cha Msomera Kata ya Misima wilayani Handeni
kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Julius Kalolo akieleza mpango wa wakala huo katika Kijiji cha Msomera
Kata ya Misima wilayanai Handeni mara baada ya kumaliza ziara ya
kukitembelea kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta
na kulia ni Mbunge wa Jimbo la  Handeni Vijijini John Salu
Mkurugenzi wa REA Mhandisi Hassan Saidi akizungumza jambo wakati wa
ziara hiyo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta
Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) John Salu akizungumza wakati wa ziara hiyo
KATIBU Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta akizungumza wakati wa
ziara hiy o kulia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini John Salu


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Julius Kalolo akitoka kwenye moja ya makazi wa wananchi wa Msomera
waliotoka Ngorongoro wakati wa ziara yake  wa kwanza kushoto ni Katibu
Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta

NA OSCAR ASSENGA,HANDENI

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam
Malima amempongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) Julius Kalolo na Watendaji wa Wakala huo kwa kazi
nzuri wanayoifanya kwa sababu imekuwa ni sekta inayotolewa mfano kwa
Afria nzima kutokana na utendaji wao.

RC Malima aliyasema hayo
wakati Mwenyekiti huyo wa Bodi ,Mkurugenzi wa REA na watendaji wengine
walipofika kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga kabla ya kuanza ziara ya
kutembelea Kijiji cha Msomera kilichopo wilayani Handeni ili kujionea
maendeleo na hali halisi na ili kupata taarifa zitakazoiwezesha bodi
kukaa na kuiridhisha mambo muhimu na ya msingi ambayo yatafanya
mazingira ya makazi kuwa na mazuri.

Alisema kwamba kutokana na
kazi nzuri inayofanywa na wakala huo na kuwa mfano kwa Afrika Nzima zipo
taasisi zinatamani kuja kujifunza kazi nzuri mlivyofanya hivyo nitumie
fursa hii kuwapongeza sana huku akiwataka kuendeleza kasi hiyo.

“Lakini
nichukue ahadi kwamba hao wakandarasi mnaofanya kazi na gharama za
vifaa vinavyotumika sio ndogo huu ni uwekezaji mkubwa ambao unafanywa na
serikali faida ni wananchi kupata umeme,niwapongeza isipokuwa miradi
hiyo ina kipindi cha miwezi 18 wamepewa niwaambie kwamba Serikali ya
Mkoa itaendelea kushirikiana nayi kusimamia miradi hii”Alisema

“Katika
kikao chetu cha leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) na Mtendaji Mkuu wa Rea na wakandarasi wa miradi
mbalimbali inayotekelezwa na REA mkoa huo tumepata muda wa kukaa na
kushauriana nasuala mbalimbali ya utekelezaji bora wa miradi ya hii
kwenye mkoa huo “Alisema

Aidha alisema wapo wanahabari hivyo
niwaambie kwenye kazi mbalimbali zinazoendelea hakuna wilaya
ilitakayokosa mradi wa rea hilo ndio kubwa na wanamshukuru Rais Samia
Suluhu,Wizara ya Nishati na REA kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha
nchi nzima huduma ya umeme inafika kwa wananchi.

Awali
akizungumza wakati akiwa eneo la Msomera wilayani Handeni Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Wakili Julius
Julius Kalolo alisema kwamba Serikali wa kuomba baadhi ya watu wa
Ngorongoro kuhamia eneo hilo kwa vyoyote mahitaji ya nishati vijijini
yamekuwa makubwa kuliko ambavyo walivyokuwa wametengeneza kwenye bajeti
yao.

Alisema hivi sasa wataweze kupitisha bajeti ya nyongeza
kuhakikisha miundombinu ya nishati katika eneo la Msomera inakwenda
vziuri kwa kuzingatia mfumuko wa wakazi wa eneo hilo ilikuwa lazima
yeye na Mkurugenzi wa REA na watendaji wafika waone hali halisi na
kupata taarifa kamili ili kuiwezesha bodi kwenye kukaa na kuiridhisha
mambo muhimu na ya Msingi.

“Tutafanya mazingira ya makazi kuwa
na mazuri na hawatawapa shida kwani wakazi walioamua wenyewe kuhamia
eneo hili ili wasione kama wametengwa kilio cha muda mrefu maeneo yake
mengi hayana huduma ya nishati vijijiji kwa kuwa hili lilijitokeza
wakaona huu ndio wakati wake waende wajione ili waweze kutimiza azma ya
kueneza nishati vijijini.

“RC ametupa maagizo ambayo tutakuwenda
kuyafanyia kazi kuhakikisha nishati ya umeme inafika Kijiji cha Msomera
na maeneo mengine hapa na hii ni hatua ya kwanza lakini bado kuna hatua
nyengine ikiwemo mpango mwengine wa kuleta nishati mbadala kwa ajili ya
kupikia ili kurahisisha maisha ya waakzi wa eneo hilo”Alisema

Naye
kwa upande Mkurugenzi wa REA Mhandisi Hassan Saidi alisema wamefika
eneo la Msomera ambacho kimetengwa kwa watanzania kutoka Ngorongoro
Arusha na Taasisi mbalimbali zipo hapo kwa ajili ya kutoa huduma na wao
wameona wahusike kuboresha huduma ya umeme kutoka kila kilomita 30 na
tayari kilomita 15 zimeshakamilika na tano za hapa zimekamilika na
Transoma ipo tayari kuwashwa na mradi utaendelea katika maeneo hayo ya
msomera.

Mhandisi Hassan alisema mradi ambao wameufanyia kazi ni
wa awamu ya tatu mzunguko wa pili kama alivyosema Mwenyekiti huo mradi
upo kila kijiji kilipewa kilomita 1 ukiangalia hiyo haitoshi lakini azma
yao ni kufikisha huduma ya umeme kwenye vijiji.

Alisema mpango
wake ni kuhakikisha vijiji vyote vya Tanzania Bara vinafikishiwa umeme
azma ya kwanza ni kufikisha umeme kwenye vituo vikubwa na kusambaza
umeme kwenye majumbani wanafanyia kaz.

Hata hivyo alisema
serikali imehaidi kuwapatia fedha hivyo wananchi wasiwe na hofu kila
kijiji kitapata umeme na wanatarajia kufikia wateja wengi zaidi na kwa
mkoa wa Tanga zaidi ya mradi wa Rea 111 ,11 wana mradi wa ujazilizi.

About the author

mzalendoeditor