Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA:’SERIKALI INAENDELEA KUTAFUTA MIKOPO KWA AJILI YA WANAFUNZI WA VYUO VYA KATI NA UFUNDI NCHINI’

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza  leo Juni 13,2022 wakati akifunga maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof. Adolf Mkenda,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifunga Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika  leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

SEHEMU ya Viongozi pamoja na Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani)  wakati akifunga maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

Mhadhiri Msaidizi na Afisa Udahili kutoka Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika,Samuel  Marandu,akimwelezea Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,Kozi zinazopatikana katika chuo hicho baada ya kutembelea Banda la Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika  wakati akifunga  Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika Uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akifurahia jambo mara baada ya kutembelea Banda la Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati akifunga  Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika Uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kutafuta mikopo kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi wa vyuo vya kati na ufundi nchini.

Hayo ameyasema leo Juni 13,2022 wakati akifunga maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Prof.Mkenda amesema kuwa  serikali inaendelea kufanya ni kutafuta mikopo na benk ya NMB imekubali kutoa sh. bilion 200 kwa ajili ya kukopesha wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati na ufundi nchini.

“Mikopo hii haitakuwa kama ile inayotolewa na Bodi ya Mikopo kwahiyo kama ni mfanyakazi atahitaji kumsomesha mtoto wake VETA atapewa mkopo huo kwa masharti nafuu”amesema Waziri Mkenda

Prof.Mkenda amesema kuwa katika kuhakikisha zoezi la kutoa mikopo katika ngazi hiyo linakuwa kwa ufasaha inahitajika kuwa na takwimu mahusus za vyuo vyote vinavyotoa mafunzo.

“Tukiwa na takwimu sahihi tukajua ni kozi gani ambazo wanafunzi wakisoma wanaajiriwa haraka tunaweza kuongea na benk zetu wakatoa mikopo kwa wanafunzi hao na watarejesha wenyewe pindi watakapo ajiriwa au kujiajiri hii itasaidia kupanua wigo wa wanafunzi wanaomaliza vyuo na kujiajiri au kuajiriwa,”amefafanua

Aidha ameliagiza Baraza la Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya UFUNDI Stadi (NACTVET) kuhakikisha wanasimamia maudhui yanayotolewa katika vyuo ili kuendelea kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutuba bunge.

“Rais Samia wakati akihutubia bunge aliagiza wizara ya Elimu kupitia sera na mitaala ya elimu ili kuongeza ubora wa elimu kuhakikisha elimu inayotolewa inaleta ujuzi ilikumuandaa muhitimu kumudu mazingira ili aweze kuajirika na kujiajiri,”amesema

About the author

mzalendoeditor