Featured Kitaifa

WAZIRI NDALICHAKO ASHIRIKI MKUTANO WA 110 WA KAZI WA KIMATAIFA NCHINI USWISI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kulia) akishiriki Mkutano wa 110 wa Kazi wa Kimataifa Juni 7, 2022 Geneva, Uswisi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Chama cha Waajiri Nchini, Bi. Suzanne Ndomba Doran, Naibu Mkuu wa Kituo Jiji la Geneva, Balozi Hoyce Temu. Kulia ni rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamhokia. 

***************************

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongoza ujumbe wa nchi katika Mkutano wa 110 wa Kazi wa Kimataifa leo Juni 7, 2022 Geneva, Uswisi.

Aidha, Waziri Ndalichako ameshiriki pia kikao cha kundi la Afrika ambapo ametoa salamu za nchi na kuwaalika nchi wanachama wa Afrika na Duniani kote kutembelea nchi ya Tanzania kwa lengo kujionea Vivutio vya kitalii na shughuli za ustawi wa wananchi zinazotekelezwa vizuri na Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

About the author

mzalendoeditor