Featured Kitaifa

WANADODOMA WAHIMIZWA KUTUNZA MAZINGIRA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya akishiriki zoezi la upandaji miti katika kuadhimisha wiki ya mazingira Duniani

Chief Mazengo akishiriki katika zoezi la upandaji miti katika kuadhimisha wiki ya mazingira Duniani.

Meneja Msaidizi Maendeleo ya Rasilimali za Misitu (TFS) Kanda ya Kati Patricia Manonga akitoa maelekezo ya namna ya kupanda miti katika kuadhimisha wiki ya mazingira Duniani.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya (aliyevaa track suit ya blue) akicheza muziki wa asili kwenye maadhimisho ya wiki ya mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya akikabidhi cheti cha pongezi kwa kikundi cha CHAPAKAZI kwa kuwa wadau wazuri wa mazingira mkoani Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya akikabidhi cheti cha pongezi kwa Bw. Ahidi Sinene kwa kuwa mdau mzuri wa mazingira ambaye ameongoza kwa kupanda miti mingi zaidi kwa mwaka huu mkoani Dodoma.

…………………………………..

Na Bolgas Odilo, Dodoma.

Wananchi Mkoani Dodoma wahimizwa kuendelea kuyatunza mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Hayo yamesemwa leo Juni 4,2022 na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya wakati akizungumza na wananchi kwenye maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani.

Msuya alisema kuwa walimu wahakikishe wanawapa wanafunzi elimu ya mazingira ili wawe mabalozi wazuri kwa kuwa wao ndio wanaunda Taifa la kesho.

“Niwaombe sana ndugu zangu tuendelee kuyatunza mazingira ili nayo yaendelee kututunza.

“Tukiyaweka mazingira safi na salama itakuwa ni faida kwa kizazi hiki cha sasa ata cha baadae.

“Niwahimize sana walimu wahakikishe wanamkabidhi kila mwanafunzi mti wake ambao atauhudumia,” alisema Msuya.

Naye Meneja Msaidizi Maendeleo ya Rasilimali Misitu (TFS) Kanda ya Kati Patricia Manonga alisema kuwa wao kama Taasisi wanatoa miche ya miti bure kwa yeyote atakayekuwa tayari kupanda na kuhudumia.

Manonga aliyasema hayo ikiwa ni moja kati ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya kutaka Dodoma ya Kijani.

“Tuna viunga vyetu vya miti ambavyo vinazalisha miche mingi kwaajili ya kupandwa maeneo tofautitofauti.

“Miche hii ya miti inatolewa bure kwa mwananchi yeyote atakayekuwa tayari kupanda na kuihudumia.

“Toka tuanzishe programu hii ya upandaji miti sisi kama taasisi tumeshapanda zaidi ya miti milioni tano.

“Hii ni hatua nzuri na niwasihi tu wananchi wenzangu kuwa tuendelee kuyatunza mazingira yetu,” alisisitiza Manonga.

About the author

mzalendoeditor