Featured Kitaifa

DC TANGA AIPONGEZA TANGA UWASA

Written by mzalendoeditor

 

Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Tanga(Tanga UWASA)Devotha Mayala akitoa
maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alipotembelea banda
lao kwenye maonyesho ya Biashara.

Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Tanga(Tanga UWASA)Devotha Mayala akitoa
maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alipotembelea banda
lao kwenye maonyesho ya Biashara

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MKUU
wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameipongeza Mamlaka ya Maji na
Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kutokana na jitihada kubwa
wanazofanya katika kutatua kero za maji kwa wananchi kwa kuendelea kutoa
huduma nzuri na bora

Alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea
banda la mamlaka hiyo kwenye maonyesha ya 9 ya biashara na utalii
yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako Jijini Tanga

Pongezi za
Mkuu huyo wa wilaya ya Tanga zimatokana na kazi kubwa inayofanywa na
mamlaka hiyo kuhakikisha huduma ya maji safi inapatikana sambamba na
kutoa taarifa kwa wananchi.

Alisema Tanga Uwasa wamekuwa
wakifanya vizuri katika utoaji wa huduma mbalimbali wanazotoa ikiwemo
kuzipatia ufumbuzi kwa haraka changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza.

“Tanga
Uwasa hatuna shida sana na nyie kazi yenu nzuri lakini zingatieni
kupitia kwenye mitaro ya maji machafu mara kwa mara… wekeni ratiba kama
kuna changamoto ziweze kutatulika kwa wakati”Alisema Mgandilwa

Awali
akizungumza Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devotha Mayala alisema kuwa
katika maonyesho hayo wamekuwa wakiwapa elimu wananchi juu ya matumizi
sahihi ya maji wawapo majumbani.

About the author

mzalendoeditor