Featured Kitaifa

WATANZANIA  WATAKIWA KUTUNZA NA KULINDA VYANZO VYA MAJI

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprica Mahundi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati  akitoa tamako la Wizara ya Maji kuhusu ushiriki wake katika maadhimisho ya siku mazingira Duniani.

BAADHI ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprica Mahundi,wakati  akitoa tamako la Wizara ya Maji kuhusu ushiriki wake katika maadhimisho ya siku mazingira Duniani.

………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprica Mahundi, amewataka Watanzania kutunza vyanzo vya maji nchini ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Mahundi,ameyasema hayo jijini Dodoma wakati  akitoa tamako la Wizara ya Maji kuhusu ushiriki wake katika maadhimisho ya siku mazingira Duniani.

.Mhandisi  Mahundi ,amesema kuwa Wizara ya Maji ni mdau mkubwa wa mazingira na maji ni rasilimali adhimu ambayo haina mbadala, hivyo inapaswa kutunzwa na kuendelezwa.

“Kutunza mazingira pamoja na rasilimali zinazozunguka kama rasirimali maji ni jukumu letu sote kwa kuwa Tanzania ni moja tu hakuna mbadala wa Tanzania.

“Kama mnavyofahamu maji ni moja ya rasilimali adhimu, maji ni uhai, maji hayana mbadala, hivyo kaulimbiu ya mwaka huu inahimiza kutunza vema rasilimali tuliyonayo ili kulinda Tanzania yetu”amesema Mhandisi Mahundi

Mhandisi Mahundi amesema kuwa hifadhi ya vyanzo vya maji ni muhimu ili kuwa na uhakika wa upatikajai wa maji kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Kaulimbiu inakwenda sambamba na tamko la Rais Samia Suluhu Hassan alilotoa tarehe 22 Machi 2022 jijini Dar es Saalam, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Maji kwamba Watanzania kutunza mazingira hususani uoto wa asili kwa kuepuka kukata au kuchoma miti ovyo”amesema.

Hata hivyo Mahundi ameziagiza taasisi zote zilizopo chini ya Wizara ya Maji kushiriki ipasavyo katika ngazi zote za jamii na kuzitaka taasisi hizo zishirikiane na wadau mbalimbali katika kusimamia utunzaji wa rasilimali za maji na kuondokana na mtazamo wa kuziachia Bodi za Maji za Mabonde pekee kusimamia na kutunza vyanzo vya maji.

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni tarehe 5 Juni, 2022 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maadhimisho haya yatafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor