WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa warsha ya maafisa mazingira wa mikoa, wilaya na Halmashauri zote nchini wenye lengo la kubadilishana uzoefu na kukumbushana kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira duniani kitakachofanyika Juni 5, Mwaka huu jijini Dodoma.
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Kanda ya kati, Dk.Franklin Rwezimula,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa warsha ya maafisa mazingira wa mikoa, wilaya na Halmashauri zote nchini wenye lengo la kubadilishana uzoefu na kukumbushana kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira duniani kitakachofanyika Juni 5, Mwaka huu jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mda mbalimbali wakati wa warsha ya maafisa mazingira wa mikoa, wilaya na Halmashauri zote nchini yenye lengo la kubadilishana uzoefu na kukumbushana kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira duniani kitakachofanyika Juni 5, Mwaka huu jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua warsha ya maafisa mazingira wa mikoa, wilaya na Halmashauri zote nchini wenye lengo la kubadilishana uzoefu na kukumbushana kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira duniani kitakachofanyika Juni 5, Mwaka huu jijini Dodoma.
…………………………….
Na Bolgas Odilo -DODOMA
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka Maafisa Mazingira nchini kutunza na kuhifadhi nyanzo vya maji lengo likiwa ni kutunza mazingira kwa vitendo.
Akiwasilisha mada leo Juni 6,2022 jijini Dodoma wakati wa warsha ya Maafisa Mazingira wa Mikoa,Wilaya na Halmashauri zote nchini ,Meneja wa NEMC, Kanda ya Kati, Dk.Franklin Rwezimula, amesema kuwa maeneo mengi ya vyanzo vya maji nchini yamekumbwa na tatizo la uvamizi wa wafugaji na wakulima wakitafuta maji kwa ajili ya kunywesha mifugo na kilimo.
Dk.Rwezimula, amesema katika warsha hiyo watajadiliana mambo mbalimbali ikiwemo Sera ya Mazingira ya mwaka 2021 ambapo NEMC watawasilisha mada mbalimbali.
‘Licha ya kuwapo na Sheria za usimamizi wa vyanzo vya maji (Bahari, Maziwa, Mito, Mabwawa na Chemichemi), kumekuwapo na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli za binadamu zinazofanyika bila kuzingatia Sheria zinazosimamia mazingira na rasilimali maji.’
Amesema kuwa NEMC pamoja na Maofisa hao wamejipanga kwenye utekelezaji wa majukumu yao kusimamia Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021.
“Tutakuwa na mada za kuwasilisha ikiwemo uharibifu na utunzaji wa vyanzo vya maji ambapo ni utekelezaji wa Dera za Mazingira pamoja na Sheria ya Mazingira ya mwaka 2014 lakini ni utekelezaji wa maagizo aliyotoa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango wakati anazindua sera ya Mazingira tarehe 12 mwezi wa pili,”amesema
Amesema NEMC wamejiandaa na baadae kupitia kikao hicho watatoka na mkakati wa pamoja ya jinsi ya kutunza mazingira kwani utunzaji wa vyanzo vya maji ni muhimu.
“Vyanzo vya maji vina umuhimu mkubwa mojawapo ni katika umeme na matumizi ya nyumbani na kilimo pamoja na mashambani, bila maji hakuna maendeleo ili tuwe na maendeleo endelevu ni lazima tuwe na maji safi na salama,”amesema.
Hata hivyo amewakaribisha wakazi wa Dodoma kufika katika banda la NEMC lilopo katika viwanja wa Jakaya Kikwete ambapo hapo watapatiwa elimu jinsi ya kutunza mazingira.
Naye, Ofisa Mazingira kutoka Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Bakari Bakari, amesema kuwa wapo tayari kuhakikisha mazingira na vyanzo vya maji vinatunzwa kwa kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.
“Kwani mazingira ni jambo mtambuka.Tupo bega kwa bega kuhakikisha mazingira yanatunzwa kama Mkoa wa Kigoma ambao una Wilaya 8 tupo bega kwa bega na Rais Samia ikiwa ni kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri,” amesema.
Awali, akifungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa, ametaka maendeleo ya watu lazima yaendane na utunzaji mazingira nchini.
“Ni lazima tupeleke uelewa kwa wananchi ili na wao wajue kuwa suala hilo la utunzaji mazingira ni la kila mtu, si la Ofisa Mazingira mwenyewe na kuwa na mikakati endelevu itakayoendana na maendeleo na uchumi wa nchi, hivyo lazima tuwe na mikakati ya kutoa elimu ka umma ili liwe jambo la watanzania,”amesema Bashungwa