Featured Michezo

WYDAD CASABLANCA YAICHAPA AL AHLY NA KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA 2022

Written by Alex Sonna

WYDAD  Athletics wamefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Mfalme Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Mabao yote ya Wydad yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco, Zouheir El-Moutaraji mwenye umri wa miaka 26, moja kila kipindi, la kwanza dakika ya 15 na la pili dakika ya 45.

About the author

Alex Sonna