Featured Michezo

COASTAL UNION WATIMIZA AHADI YA RC ADAM MALIMA

Written by mzalendoeditor

Wachezaji
wa Coastal Union wakiwania mpira dhidi ya wa Azam FC wakati wa mechi ya
nusu fainali ya Kombe la FA iliyopigwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja
wa Sheirh Amri Abeid Jijini Arusha ambapo Coastal Union ilishinda

NA OSCAR ASSENGA,ARUSHA

MATOKEO ya UshindI walioupata kwa Penalti 6
kwa 5 hadi kuitoa Azam FC kwenye tumaini la kucheza Fainali za Kombe la
Shirikisho ni kama sehemu ya Kikosi cha Coastal Union ya Tanga
wametimiza Ahadiwaliyoitoa kwa Mkuu wao wa Mkoa Adam Malima.
 

Kabla
ya mchezo huo wa nusu fainali za FA kati ya Coastal dhidi ya Azam, Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alitembelea Kambi yA Wagosi wa Kaya huko
Mbauda Jijini Arusha.

Katika mazungumzo yake na wachezaji Malima aliwaeleza kuwa wana kila
sababu ya kuifunga Azam kwa madai kuwa wameshawahi kucheza nao huku
wakiweza kuonyesha kiwango kikubwa mchezoni.

Mbali na hayo Malima alisema, Kikosi hicho cha Coastal kitakapoibuka
kidedea kwenye mchezo huo kitaleta sifa njema kwa Mkoa huku
akitumiafursa hiyo kuwapatia wachezaji donge nono.

“Najua nina deni lenu niliahidi na nitawapa hata hivyo mchezo huu
mnapaswa kushinda na nitawapa kiasi kingine cha fedha”alisikika RC
Malima akiwapa morari wachezaji wa Coastal.

Baada ya kusema hayo, nahodha wa Coastal Amani Kyata alimhakikishia Mkuu
wa Mkoa Adam Malima kwamba wataishinda Azam kwenye mchezo huo.

Coastal imeifunga Azam kwa Penalti 8 kwa 5 ambapo sasa timu hiyo yenye
maskani yake barabara 11 Jijini Tanga itacheza Fainali na Dar Young
African.

NGOMA ya Baikoko imeonekana kuwa Nyenzo waliyoitumia Mashabiki wa
Coastal katika kuwapa nguvu Wachezaji wao na hivyo kukiwezesha Kikosi
cha Wagosi wa Kaya kutinga Fainali za Kombe la FA.

Kabla ya mchezo wa nusu fainali kupigwa, majira ya asubuhi mashabiki wa
Coastal waliteka Viunga vya Jiji la Arusha kwa kupiga na kucheza ngoma
yao ya Baikoko.

Kitendo hicho cha kuzunguka wakitumbuiza kwa ngoma hiyo mitaani huku 
wakionyesha vidole vitatu kama ishara ya ushindi hatua ambayo ilionekana
kuleta furaha kwa wapenzi wengi wa soka.

Pamoja na kuzunguka mitaani kwa shangwe, mashabiki hao walihamia mtaa
wa Mbauda walikofikia Coastal na kulakiwa na wachezaji ambao nao
walionekana kuwa na ari ya ushindi.

Shangwe na nderemo zilihamia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa mashabiki
kupiga ngoma ya Baikoko wakiishangilia timu yao wakati ikicheza hadi
ilipoibuka mshindi.

Mchezo ulikuwa wa vuta nikuvute kwa timu zote kushindwa kupata mabao
hadi dk 90 zilipomalizika na kuongezwa dk 30 nazo zikamalizika kwa
sare hadi ilipofika hatua ya Mikwaju ya Penalti.

About the author

mzalendoeditor