Featured Kitaifa

WAZIRI MCHENGERWA ATEMA CHECHE KWA VIONGOZI WA MICHEZO,ATAKA WABADILIKE

Written by mzalendoeditor


Waziri
wa Utamaduni,Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa akizungumza
wakati wa akifunga kikao kazi cha viongozi wa vyama na mashirikisho ya
michezo nchini kilichoratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni,Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa amewataka 
viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini kutotumia taasisi
wanazoziongoza kujinufaisha kwa  vipato tu na badala yake wawe wabunifu
na wazalendo ili kuleta  mapinduzi kwenye  michezo  na kuendana  na
maono ya Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu
Hassan ya kutumia michezo kuleta uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa
ujumla.
 Mhe.
Mchengerwa ameyasema haya leo Mei 27, 2022 wakati akifunga  kikao kazi
cha viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini 
kilichoratibiwa  na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufuatia  maelekezo
yake aliyoyatoa wakati akiisimika Bodi  ya BMT hivi karibuni ya kutaka
kuwa na utawala bora kwenye vyama na mashirikisho ya michezo ili
kuendeleza michezo.
 Mhe.
Mchengerwa amefafanua kuwa yapo  mataifa  mbalimbali duniani ambayo 
hayana miundombinu ya michezo na  yana idadi ndogo ya watu
ukilinganisha  na Tanzania  lakini yamekuwa yakifanya  vizuri kwenye 
michezo hivyo amewataka kubadili fikra  potofu ili wanaowaongoza waige 
mifano kutoka  kwao hatimaye kuleta mapinduzi makubwa kwenye michezo. 
 “Hatutaweza
kupiga hatua kwenye michezo kama   sisi viongozi hatutaweza kubadilika
na kuendelea kuwa na fikra potofu ya kudhani vyama na mashirikisho ni
mahali pa kujipatia vipato tu. Nawaomba tubadilike mimi katika kipindi
changu sitaweza kuruhusu kutokea hayo. Mpango wa matumauni ya kesho
lazima tuanze kujenga leo”. ameongeza Mhe. Mchengerwa.
Amesema
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
imeelekeza nguvu kubwa kuendeleza sekta za utamaduni, Sanaa na Michezo
ndiyo maana iliunda upya Wizara hii ili iweze kujitegemea, kuongeza
bajeti, kutoa punguzo kwenye nyasi bandia ili kuimarisha viwanja vya
soka pamoja na kuanzisha mfuko wa maendeleo ya michezo.
Ameongeza
kuwa mfuko huo umepewa chanzo madhubuti ambacho  ni fedha za asilimia
tano ya mapato yatokanayo na michezo ya kubashiri matokeo ya michezo.
Kikao
hicho pamoja na mambo mengine kimejadili kwa kina vigezo   vya muongozo
wa kusaidia timu za taifa  kwa kutumia fedha za mfuko wa maendeleo ya
michezo na kuja na mawazo ambayo yatafanyiwa  kazi na serikali ili kuwa
na uwazi katika usaidiaji wa  timu hizo katika michezo mbalimbali.  
Aidha,
amewasihi viongozi hao kufuata  miongozo na taratibu za nchi  sambamba
na kuziheshimu  mamlaka  na taasisi zinazosimamia michezo nchini, 
kuimarisha  utawala bora na weledi  katika kazi.
Mambo mengine ni pamoja na kuimarisha eneo la utaalamu na taswira za    taasisi zao kwa kuwa na mikakati yenye dira.
Ameeleza
kuwa Serikali itaendelea kujenga miundombinu mipya na ya kisasa ya
michezo ambapo kwa upande wake Naibu Waziri, Mhe, Pauline Gekul
amewataka wadau washirikiane na kupendana ili kuongoza kwa mafanikio.
Naye
Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi amewataka viongozi hao kuwa wabunifu wa
kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato badala ya kutegemea Serikali

About the author

mzalendoeditor