Featured Kitaifa

RUWASA KAHAMA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA,YAANIKA MAFANIKIO LUKUKI

Written by mzalendoeditor
 

 

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini wilayani Kahama kwenye mkutano wa pili wa mwaka wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii leo Alhamisi Mei 26,2022 katika ukumbi wa Green Angel Mjini Kahama

 

Afisa Tarafa ya Mweli wilaya ya Kahama  Salakana Japhet Peter akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga umefanya Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama kwa ajili ya kujadili uelewa, kutathmini na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira.
 
 
Mkutano huo umefanyika leo Alhamisi Mei 26,2022 katika ukumbi wa Green Angel Mjini Kahama na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maji na usafi wa mazingira wilayani Kahama.
 
 
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini wilayani Kahama , Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili amesema hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa hivi sasa katika eneo linalohudumiwa na RUWASA Kahama ni asilimia 66, sawa na watu wapatao 490,813 ya wakazi wote 742,521 waliopo vijijini, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.8 kutoka asilimia 54.2 iliyokuwepo hadi Juni 2019.
 
“Hii ni baada ya kukamilisha miradi ya maji iliyokuwa inatekelezwa kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2019/2020 na 2020/2021, kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi. Baada ya kukamilika kujengwa miradi yote inayoendelea kutekelezwa kwa sasa, kiwango cha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kinatarajiwa kupanda hadi asilimia 74.6 ifikapo Machi 2023”,amesema.
 
“Ili kuwa na usimamizi imara wa miradi ya maji vijijini na kwa mujibu wa Sheria ya Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na.5 ya mwaka 2019, hapo awali viliundwa Vyombo vya Kutoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) 29 lakini kutokana na changamoto za kiuendeshaji, Vyombo hivyo vimeunganishwa na kuunda Vyombo Jumuishi na hivyo kwa sasa kuna Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii vilivyosajiliwa 13. Kulingana na muundo mpya wa CBWSO, kila CBWSO inapaswa kuwa na Kamati Tendaji ambayo inajumuisha Fundi na Mhasibu. Kwa sasa CBWSO 9 ndiyo zenye Kamati Tendaji”,ameeleza Mhandisi Magili.
 
 
Aidha katika bajeti ya kipindi cha mwaka 2021/2022, RUWASA Wilaya ya Kahama ilipanga kutekeleza miradi ipatayo 26 katika Halmashauri zote tatu (3), ambapo miradi 5 ni ya ukamilishaji na miradi 21 ni mipya, ambayo inajumuisha pia miradi ya utafutaji wa vyanzo vipya vya maji. Miradi yote ilitengewa bajeti ya kiasi cha Sh. 8,842,298,094.64.
 
“Hadi Aprili 30, 2022, fedha zilizotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ni kiasi cha Sh. 6,685,419,189.60, sawa na asilimia 75.6. Hadi sasa, kati ya miradi 5 ya ukamilishaji, miradi 3 imekamilika na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi, miradi hiyo ni mradi wa maji wa Mhangu – Ilogi ambao umeanza kutoa huduma ya maji katika kijiji cha Ilogi, mradi wa maji wa Nyankende na mradi wa maji wa Igunda”,amesema Mhandisi Magili.
 
 
“Utekelezaji wa bajeti hii unakwenda sambamba na utekelezaji wa miradi ya maji kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Athari za UVIKO – 19. Miradi hiyo inatekelezwa katika vijiji vya Mwashigini (Msalala) na Itumbili (Ushetu) na inatarajiwa kukamilika kabla au ifikapo Juni 30, 2022. Miongoni mwa miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa katika kipindi cha mwaka 2021/2022, ni miradi ya maji ya bomba”,ameongeza Magili.
 
 
Amesema miradi mingine ni pamoja na utafutaji wa vyanzo vipya vya maji katika maeneo mbalimbali ikiwemo Utafutaji wa vyanzo vya maji chini ya ardhi katika vijiji vya Izumba, Ndala, Nundu, Jomu na Ndalilo, Utafutaji wa vyanzo vya maji chini ya ardhi katika vijiji vya Ubagwe, Chona, Kinamapula, Uyogo, Bukomela, Makongolo, Busenda and Nyalwelwe na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria katika kata 11 za Bukomela, Igunda, Kisuke, Kinamapula, Mapamba, Mpunze, Nyamilangano, Ukune, Ulowa, Mbika na Uyogo.
 
 
Amezitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika utekelezaji wa majukumu ya RUWASA Kahama ni pamoja na Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, Ukosefu wa vyanzo vya maji vya uhakika kwenye baadhi ya maeneo, hususani katika maeneo ya Halmashauri ya Ushetu, Ubovu wa miundombinu, hususani uchakavu katika mitandao ya mabomba kwenye miradi ya zamani na Matumizi madogo ya maji, hususani wakati wa masika na kusababisha baadhi ya CBWSO kushindwa kujiendesha.
 
 Akifungua Mkutano huo, Afisa Tarafa ya Mweli wilaya ya Kahama Salakana Japhet ameipongeza RUWASA Kahama kwa juhudi inazoendelea nazo katika kuwafikia wananchi na kuwapatia huduma ya maji safi na salama.
 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga ameishukuru RUWASA kwa kutekeleza vizuri Ilani ya Uchaguzi CCM na kumshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu kuleta fedha nyingi ili kuhakikisha miradi inatembea na wananchi wanapata maji safi na salama huku akiomba juhudi na bidii zaidi ziongezwe kwenye sehemu ambazo maji hayajafika.
 
“Naomba tuongeze kasi kwani wananchi wanahitaji maji safi na salama kwenye maeneo yetu ili kuondokana pia na maradhi yakiwemo magonjwa ya matumbo, CCM inaridhika na namna Ilani inavyotekelezwa…Naomba mkaongeze kasi kwenye vyanzo vya maji vitunzwe, miti itunzwe ili watu wetu wapate maji…Tuhakikishe vyanzo vya maji vinatunzwa,miti inapandwa”,amesema Myonga.
 
 
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu Mhe. Gagi Lala amewapongeza RUWASA kwa kufanya kazi vizuri huku akiomba maji ya Ziwa Victoria yafike Ushetu kwani kimekuwa kilio cha muda mrefu na wamekuwa wakiahidiwa mara kwa mara kuhusu suala la Maji ya Ziwa Victoria lakini hakuna suluhisho.
 
“Halmashauri ya Ushetu na idadi kubwa ya wananchi..Sisi hatuna hata tone moja la maji ya Ziwa Victoria, tunaomba na sisi tupewe maji ya Ziwa Victoria kwani mahitaji ya maji ni makubwa..Naomba serikali isikie kilio chetu, tunahitaji maji Ushetu”,amesema Lala.
 
Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Masasila Maduka amesema tayari serikali imesikia kilio cha wananchi wa Halmashauri ya Ushetu.
 
 “Suala la Ushetu serikali imeshasikia. Changamoto ya Ushetu ni upatikanaji wa maji chini ya ardhi ni mdogo, kwa kutambua hilo serikali imetangaza zabuni ya Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kufanya usanifu, muda wowote atapatikana. Serikali inataka ianzishe chanzo kipya ambacho kipo halmashauri ya Nyang’hwale kwa ajili ya kuyapeleka Ushetu. Baadae serikali itatangaza Mkandarasi wa kutekeleza mradi huo na wakati tunasubiri maji ya Ziwa Victoria tunaendelea na mpango wa kuchimba visima virefu”,amesema Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Masasila Maduka.
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Tarafa ya Mweli wilaya ya Kahama Salakana Japhet  Peter akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama kwa ajili ya kujadili uelewa, kutathmini na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira leo Alhamisi Mei 26,2022 katika ukumbi wa Green Angel Mjini Kahama. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini wilayani Kahama kwenye mkutano wa mwaka wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii leo Alhamisi Mei 26,2022 katika ukumbi wa Green Angel Mjini Kahama
Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Masasila Maduka  akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama 
Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Masasila Maduka  akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama 

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu Mhe. Gagi Lala akiipongeza RUWASA kwa kufanya kazi vizuri huku akiomba maji ya Ziwa Victoria yafike Ushetu “Sisi hatuna hata tone moja la maji ya Ziwa Victoria, tunaomba na sisi tupewe maji ya Ziwa Victoria”.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kahama , Mhe. Yahya Ramadhani akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama

 

Mkuu wa Idara ya Utunzaji wa Vyanzo vya Maji Bonde la Ziwa Tanganyika Mhandisi Odemba Kornel akitoa mada kuhusu vyanzo vya maji
Afisa Vipimo kutoka Wakala wa Vipimo Mkoa wa Shinyanga Leo Patrick Thadey akitoa mada kuhusu vipimo
Wadau wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama
Wadau wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama
Wadau wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii Wilayani Kahama ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Kahama.
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
 

About the author

mzalendoeditor