Featured Kimataifa

RAIS SAMIA ATEMBELEA ENEO LA MAKUMBUSHO NA KUWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA RAIS WA KWANZA WA GHANA KWAME NKRUMAH,ACCRA NCHINI GHANA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Mnara wa kumbukumbu katika eneo la Makaburi alipozikwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah wakati alipotembelea eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) katika Jiji la Accra nchini Ghana 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah wakati alipotembelea eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) katika Jiji la Accra nchini Ghana 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama mbele ya mnara wa kumbukumbu kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah katika eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) Jijini  Accra nchini Ghana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo wakati alipotembelea katika eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) Jijini  Accra nchini Ghana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkataba wa eneo huru la Biashara Barani Afrika (The African Continental Free Trade Area), katika Ofisi za (AfCFTA)  Jiji la Accra nchini Ghana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Wamkele Mene katika Ofisi za (AfCFTA) Accra nchini Ghana.

About the author

mzalendoeditor