Featured Kitaifa

DKT CHAULA ATETA NA KAMISHNA WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula amekutana na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Fatma Khalfan katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, ukatili kwa Wazee, masuala ya Ustawi wa Jamii hasa watoto.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Fatma Khalfan ameambatana na Wakurugenzi kutoka katika Tume hiyo.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mikakati inayolenga kuboresha Ustawi wa Jamii nchini yakiwemo Makundi Maalum.

About the author

mzalendoeditor