Uncategorized

YANGA YA UBINGWA YAIDIDIMIZA MBEYA KWANZA,MAYELE,MAKAMBO WANG’ARA

Written by mzalendoeditor

VINARA Yanga wamezidi kuukaribia Ubingwa wa 28 baada ya kuichapa mabao 4-0 timu ya Mbeya Kwanza kutoka jiji la Mbeya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walianza mpira kwa kasi huku Mbeya City wakicheza kwa kushambulia na kujilinda mnamo dakika ya 34 Mzee wa kutetema baada ya kucheza mechi nne bila kutetema aliwanyanyua mashabiki wake akifunga bao kwa kichwa akimalizia pasi ya Salum Aboubakar ‘Sure Boy’.

Baada ya kupata bao hilo Yanga waliendelea kulishambualia lanngo la wapinzani dakika ya 38 Saido Ntibazonkiza alifunga bao la pili akimalizia pasi ya Khalid Aucho kabla hajaenda mapumziko Dickson Ambundo alipigilia msumari wa tatu akimalizia Pasi safi kutoka kwa Jesus Moloko dakika ya 45+2.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Yanga walifaidika na mabadiliko hayo dakika ya 73 Herieth Makambo aliwajaza Mbeya kwanza akimalizia mpira wa Chico Ushindi.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 63 huku wakihitaji Pointi 6 tu ili wawe Mabingwa wa Ligi Kuu Msimu wa 2022 na kuwaacha Simba kwa tofauti ya Pointi 13 ambao wapo nyuma kwa mchezo mmoja.

Yanga watashuka tena dimbani Mei 22,2022 katika uwanja wa CCM Kirumba kuwavaa Biashara United kabla ya kucheza nusu Fainali ya Kombe la Azam dhidi ya Simba Mei 28,2022 uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

About the author

mzalendoeditor