Featured Kitaifa

MAVUNDE AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA TAFITI ZA USHIRIKA DODOMA

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde,akizungumza wakati akifungua  kongamano la pili la Tafiti za Ushirika ambalo limeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na  Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) likiwa na lengo la kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya ushirika kupitia tafiti zilizofanyika na uzoefu wa wadau mbalimbali leo Mei 12,2022 jijini Dodoma.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dkt. Benson  Ndiege,akielezea umuhimu wa kongamano la pili la Tafiti za Ushirika ambalo limeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na  Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) likiwa na lengo la kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya ushirika kupitia tafiti zilizofanyika na uzoefu wa wadau mbalimbali leo Mei 12,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa ufunguzi wa  kongamano la pili la Tafiti za Ushirika ambalo limeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na  Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) likiwa na lengo la kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya ushirika kupitia tafiti zilizofanyika na uzoefu wa wadau mbalimbali leo Mei 12,2022 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  kongamano la pili la Tafiti za Ushirika ambalo limeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na  Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) likiwa na lengo la kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya ushirika kupitia tafiti zilizofanyika na uzoefu wa wadau mbalimbali leo Mei 12,2022 jijini Dodoma.

………………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde,amezindua kongamano la pili la Tafiti za Ushirika huku akiwataka viongozi wa vyama vya Ushirika nchini kuhakikisha ushirika unakuwa fursa badala ya  kuzalisha migogoro.

Akizungumza leo Mei 12,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la pili la Tafiti za Ushirika,Mavunde amesema kuwa,Ushirika ni eneo ambalo likitumika vyema linaweza kuisaidia nchi hata kutatua changamoto iliyopo nchini ya uhaba wa mafuta ya kula.

Kongamano hilo limeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na  Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) likiwa na lengo la kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya ushirika kupitia tafiti zilizofanyika na uzoefu wa wadau mbalimbali.

Mavunde amesema,sheria ya ushirika inatoa fursa kukabili changamoto nyingi hapa nchini ikiwemo katika kuzalisha mafuta ya kula.

Kwa mujibu wa Mvunde Serikali inatumia shilingi bilioni 474 kuagiza mafuta nje ya nchi huku akisema,lazima ushirika uwe sehemu ya utatuzi wa changamoto hii .

“Katika makongamano haya lazima muungalie ushirika katika picha tofauti ,maana huko zipo fursa za uwekezaji ,hakuna sababu ya kuzalisha migogoro kwenye ushirika ,tunataka ushirika uzalishe utajiri,

“Haipendezi kila siku kusikia kwenye ushirika ,hali hiyo lazima ikome..,kwenye ushirika kunanyooshewa vidole kwa uovu ,lazima tuutoe ushirika huko .”alisema Mavunde

Amewataka viongozi wa vyama hivyo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,uwajibikaji na uadilifu ili kuleta tija katika tasnia ya ushirika nchini.

Aidha Mavunde amewataka wajumbe wa kongamano hilo kujadili kwa kina kuona namna kongamano hilo litatoka na utatuzi wa changamoto ya mafuta ya kula iliyopo nchini,ngano na sukari ili ifike wakati bidhaa hizo zote zipatikane hapa nchini.

Awali Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dkt. Benson  Ndiege, amesema,kongamano hilo ni muhimu katika kuibua changamoto za ushirika na kuzitafutia ufumbuzi.

“Tunachotakiwa hapa ni kuibua changamoto na kuziweka kwenye utekelezaji wa mwaka unaokuja .”amesema 

“Kwa hiyo viongozi tunatakiwa kuendesha ushirika kwa mujibu wa sheria ya Ushirika.”

Akitoa maelezo ya kongamano hilo,Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Dkt.Edmund Zakayo amesema,wameamua kufanya makongamano ya tafiti za ushirika kutokana na tafiti nyingi kutokuwa na tija kutokana na tafiti nyingi kuandikwa kwa lugha ya kingereza.

Amesema,hali hiyo imefanya tafiti hizo kubaki kwenye makaratasi kutokana na lugha inayotumika katika kuyaandaa .

“Kutokana na hali hiyo ikaonekana umuhimu wa kuandaa kongamano la kwanza la tafiti za ushirika na hatimaye kuazimia kuwa na kongamano kila mwaka ili tuweze kupata fursa ya kujadiliana matokeo ya tafiti na kujadiliana changamoto zilizopo.”amesema

About the author

mzalendoeditor