Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI KATAMBI ATIMIZA AHADI KWA VIONGOZI WA BAKWATA SHINYANGA

Written by mzalendoeditor
 
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga  Mjini Samwel Jackson (kulia) akimkabidhi Katibu wa BAKWATA Mkoa wa  Shinyanga, Ally Idrissa Abeid shilingi
500,000/= zilizotolewa  na Mbunge wa
Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia
ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe.
Patrobas Katambi kwa ajili ya BAKWATA mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwel Jackson (kushoto) akimkabidhi Katibu wa BAKWATA wilaya wa Shinyanga, Ramadhani Majani shilingi
500,000/= zilizotolewa  na Mbunge wa
Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia
ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe.
Patrobas Katambi kwa ajili ya BAKWATA wilaya ya  Shinyanga.
 

 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ametimiza ahadi aliyoitoa kwa viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Shinyanga na Wilaya ya Shinyanga kuchangia shilingi Milioni moja kwa ajili ya BAKWATA.
Akikabidhi fedha hizo leo Jumanne Mei 10,2022 kwa niaba ya Mbunge Patrobas Katambi, Katibu wa Mbunge huyo Samwel Jackson amesema Mhe. Mbunge Katambi alitoa ahadi ya kuchangia shilingi 500,000/= kwa ajili ya BAKWATA wilaya ya Shinyanga na shilingi 500,000/= kwa ajili ya BAKWATA Mkoa wa Shinyanga Aprili 24,2022 wakati akifuturisha waumini wa dini ya Kiislamu na wadau mbalimbali Mkoa wa Shinyanga.
 
“Nimekuja kutimiza wajibu wangu kuleta fedha alizoahidi Mhe. Mbunge Patrobas Katambi kiasi cha shilingi 500,000/= kwa ajili ya BAKWATA wilaya ya Shinyanga na shilingi 500,000/= kwa ajili ya BWAKATA mkoa wa Shinyanga ambazo aliahidi siku ya Jumapili Aprili 24,2022 wakati akifuturisha waumini wa dini ya Kiislamu na wadau mbalimbali mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema”,amesema Jackson.
Akizungumza wakati wa kupokea fedha hizo, Katibu wa BAKWATA mkoa wa Shinyanga, Ally Idrissa Abeid amemshukuru Mbunge Katambi kwa kutekeleza ahadi yake huku akieleza kuwa mbunge huyo amekuwa akishirikiana na BAKWATA mara kwa mara katika masuala mbalimbali.
“Tunamshukuru Mhe. Mbunge Katambi kwa kutupa kipaumbele amekuwa akitushika mkono mara kwa mara. Mwaka jana pia alitufuturisha wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
 
 
Pia alitupatia shilingi milioni moja kwa ajili ya BAKWATA wilaya na Mkoa pamoja na shilingi 500,000/= kuchangia ujenzi wa msikiti…Tunamuombea kwa Mungu azidi kumuongezea zaidi na kumbariki”,amesema Abeid.

 

About the author

mzalendoeditor