Featured Kitaifa

ALIYEMWAGIWA TINDIKALI APELEKWA INDIA KUTIBIWA

Written by mzalendoeditor

Tariq Awadhi (31) leo Jumapili Mei 8, 2022 ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya macho.

Tariq ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) baada ya kumwagiwa tindikali anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa macho katika Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India.

Tariq anahitaji Sh35 milioni ili aweze kufanyiwa upasuaji wa macho katika hospitali ya Apollo.

Akizungumza na Mwananchi digital leo kabla ya kuondoka uwanja wa Ndege wa Kimataifa (KIA), Tariq amewashukuru  Watanzania waliomchangia kiasi cha Sh14 milioni.

“Nawashukuru Watanzania wenzangu ambao wanaendelea kunichagia naomba wasikate tamaa waendelee kunisaidia ili niweze kufanikiwa kurudisha macho yangu katika hali yake ya kawaida kwani maumivu ni makali.

“Mpaka sasa wananchi wameweza kunichagia kiasi cha Sh14 milioni, nawashukuru sana kwa upendo wao kwangu, naomba mzidi kuniombea ili niweze kufanikisha matibabu yangu, naamini msaada wenu na maombi yenu ni muhimu sana kwangu nawategemea sana,”amesema Tariq

Tariq ameendelea kuwaomba Watanzania na Serikali kumsaidia ili afanikishe matibabu yake

Kwa yeyote atakayeguswa kumchangia Tariq, namba zake ni 0764510774 Au Akaunti namba zake ni :3012111594790 Equity Benki kwa jina la Tariq Kipemba

CHANZO:MWANANCHI

About the author

mzalendoeditor