Featured Kitaifa

MKUTANO MKUU WA TANCCOOPS LTD WAFANYIKA SHINYANGA

Written by mzalendoeditor
Mrajisi Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Grace Mwagembe akizungumza kwenye Mkutano Mkuu  TANCCOOPS LTD kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Tanzania.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD) umefanyika Mkoani Shinyanga huku wajumbe wa mkutano huo wakiaswa kujisimamia na kuendesha  Ushirika kiushindani na kibiashara.
 
 
Mkutano Mkuu wa TANCCOOPS LTD ambao mgeni rasmi alikuwa Mrajis Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Tanzania, Grace Mwagembe umefanyika Alhamisi Mei 5,2022 katika ukumbi wa mikutano wa SHIRECU na kuhudhuriwa na wajumbe wa TANCCOOPS LTD inayoundwa na Vyama Vikuu vya ushirika 14 kutoka kwenye Mikoa inayojishughulisha zao la Pamba.
 
 
Mbali na kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha Ushirika Mkutano huo pia umeenda sanjari na Uchaguzi wajumbe wa bodi na mwakilishi nje ya bodi ya TANCCOOPS LTD ili kuziba nafasi zilizokuwa wazi ambapo Baraka Joseph Masoko – kutoka Mirambo Union na Lazaro Kidiga Walwa wamechaguliwa kuwa wajumbe wa bodi huku Daniel Mwita Masanja akichaguliwa kuwa Mjumbe nje ya bodi baada ya kupigiwa kura na wajumbe 17 wa mkutano.
 
Msimamizi wa uchaguzi huo, Mrajis Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Tanzania, Grace Mwagembe amesema mchakato wa uchaguzi umefanyika vizuri huku akisisitiza kuwa endapo mjumbe wa bodi atakayekengeuka mbele ya safari atakaa nje na nafasi yake kujazwa na mjumbe mwingine.
 
Amesema mara baada ya uchaguzi wajumbe waliochaguliwa watapewa mafunzo elekezi.
 
“Naomba Wanachama muwe na uchungu na chama ili kujenga ushirika na TANCCOOPS LTD kuwa imara zaidi. Tasnia ya pamba inavyokwenda mnatakiwa mjikaze zaidi,mfanye kibiashara”,amesema.
 
Mwagembe amesisitiza kuwa Ushirika ni biashara hivyo kuwataka viongozi wa vyama vya ushirika kuwa wabunifu wanapoongoza wenzao.
 
“Ninawaomba msiuchukulie ushirika kama pori, msijifanye wajuaji sana kwenye vitu msivyovifahamu mkaharibu mambo. Tunataka Ushirika biashara. Naomba pia mhamasishe wanawake waingie kwenye ushirika kwani waliopo ni wachache sana”,amesema Mwagembe.
 
Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace amesema Ushirika ni ushindani hivi sasa hivyo ni lazima Ushirika ujiendeshe kibiashara ili kuepuka kuchafuka.
 
“Shindaneni kibiashara hakuna mtu wa kukubeba, ukilia utalia kivyako, jipange kibiashara na yale masuala ya kwenda kiholela hayapo tena, tunatakiwa kubadilika na tufanye kwa umakini, kibiashara”,amesema Boniphace.
Mgeni rasmi Mrajis Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Grace Mwagembe akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD) kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika ( Tanzania Federation of Cooperatives – TFS), Alex Ndikilo akifuatiwa na Mwenyekiti wa TFS, Charles Gishuli.
Mgeni rasmi Mrajis Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Grace Mwagembe akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD) kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Tanzania. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika (Tanzania Federation of Cooperatives – TFS), Charles Gishuli, kulia ni Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace.
Wagombea watatu kugombea ujumbe wa bodi ya TANCCOOPS LTD wakionesha majina yao ambapo kati yao Baraka Joseph Masoko – kutoka Mirambo Union (katikati) na Lazaro Kidiga Walwa (kushoto) wamechaguliwa kuwa wajumbe wa bodi.
Mgombea nafasi ya mjumbe nje ya bodi ya TANCCOOPS LTD Daniel Mwita Masanja aliyechaguliwa kuwa Mjumbe nje ya bodi baada ya kupigiwa kura 16 za NDIYO na 1 ya HAPANA akiomba kura
Zoezi la kuhesabu uchaguzi wa wajumbe wa bodi TANCCOOPS LTD likiendelea chini ya usimamizi wa Mrajis Msaidizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Grace Mwagembe kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Tanzania ambapo Baraka Joseph Masoko – kutoka Mirambo Union na Lazaro Kidiga Walwa wamechaguliwa kuwa wajumbe wa bodi huku Daniel Mwita Masanja akichaguliwa kuwa Mjumbe nje ya bodi baada ya kupigiwa kura na wajumbe wa 17 wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD), Zainab Mahenge akifungua Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD).
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD). Kulia ni Francis Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Chato,Deogratius akifuatiwa na Mwenyekiti wa TANCCOOPS LTD), Zainab Mahenge.
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu, Kwiyolecha Nkilijiwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD) . Kulia ni Mwenyekiti wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD), Zainab Mahenge, kushoto ni Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace .
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD)
Mjumbe wa Sekretarieti na Meneja wa Singida Farmers, Ramadhan Sadick Seif akiwasilisha taarifa ya mwenyekiti wa TANCCOOPS LTD kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD). Katikati ni Meneja wa TANCCOOPS LTD, Ramadhani Kato.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika (Tanzania Federation of Cooperatives – TFS), Charles Gishuli akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD)
Francis Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Chato,Deogratius akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD). Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida, Yahaya Ramadhani.
Meneja wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika ( Tanzania Federation of Cooperatives – TFS), Alex Ndikilo akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD).
Wajumbe wakisoma makablasha kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD)
Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD)
Wajumbe wa Sekretarieti (Meneja wa Singida Farmers, Ramadhan Sadick Seif) na Meneja wa TANCCOOPS LTD, Ramadhani Kato (kushoto) wakiandika dondoo muhimu kwenye Mkutano Mkuu wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba ( Tanzania Cotton Co – Operatives Joint Enterprise Limited – TANCCOOPS LTD).
 
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 

About the author

mzalendoeditor