Featured Michezo

REAL MADRID YATINGA KIBABE FAINALI LIGI YA MABINGWA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester City usiku wa Jumatano Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid nchini Hispania.
Dakika 90 zilimaliza la Real wakishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Rodrygo yote dakika ya 90 na 90 na ushei baada ya Man City kutangulia kwa bao la Riyad Mahrez dakika ya 73.
Matokeo ya jumla yakawa 5-5 kufuatia Man City kushinda 3-2 kwenye mechi ya kwanza Uwanja wa Etihad wiki iliyopita, hivyo mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza na ndipo Mfaransa, Karim Benzema amekuwa shujaa wa Bernabeu kwa mara nyingine tena kwa bao lake la  penalti dakika ya 95 kufuatia yeye mwenyewe kuchezwa vibaya na Ruben Dias.

Kwa ushindi huo wa jumla wa 6-5, Real Madrid inakwenda Fainali itakayopigwa Mei 28 Uwanja wa Stade de France Jijini Paris na itakutana na timu nyingine ya England, Liverpool ambayo imeitoa Villarreal ya Hispania pia.

About the author

mzalendoeditor