Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AAHIDI KUIMARISHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushiriki Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika Jijini Dodoma

Wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Binafsi pamoja na Sekta mbalimbali wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoa ujumbe mbalimbali kuhusiana na Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Wafanyakazi waliokuwa wakipita mbele ya Jukwaa Kuu na ujumbe mbalimbali wa siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya wakiimba nyimbo ya Mshikamano (Solidarity)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wafanyakazi kutoka Sehemu mbalimbali nchini katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kushiriki katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

………………………………………………….

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuimarisha maslahi ya wafanyakazi nchini.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kwenye uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.

Rais Samia amesema kwa kuwa alishatoa ahadi mwaka jana, ameagiza kufanyika kwa majadiliano ya kuimarisha maslahi ya wafanyakazi yanayoendelea kati ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Serikali ili kujua kiwango cha maslahi itakayohitajika.

“Yale tuliyoyafanya mwaka huu, mambo mbalimbali, kupunguza kodi…tutaendelea kuyafanya. Lakini pamoja na hayo, lile jambo letu lipo. Ndugu zangu, jambo letu lipo si kwa kiwango kilichosemwa na TUCTA kwasababu mnajua hali ya uchumi wetu, na hali ya uchumi wa dunia. Hali si nzuri sana, uchumi wetu ulishuka chini mno.”

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameagiza Maafisa Rasilimali Watu pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kushughulikia haki na stahiki za watumishi wanaotarajia kustaafu ndani ya miezi sita ili mtumishi anapofika muda wa kustaafu, mafao yake yawe tayari. 

Kuhusu watumishi waliofanya kazi kwa muda mrefu na kisha kufukuzwa kazi kwa sababu ya vyeti vya kughushi bila kulipwa malipo yoyote, Rais Samia pia ameagiza Wizara ya Fedha na Mipango kushugulikia stahiki zao zinazotokana na makato ya mishahara yao na kuwalipa. 

Rais Samia amesema Serikali imeshaunda Bodi za Kima cha Chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi na ya Umma na tayari zimeshaanza kufanya tathmini ya mishahara iliopo sasa. 

Serikali imeendelea kustawisha maslahi ya wafanyakazi tangu mwaka 2021 ikiwemo kupunguza makato ya kodi, kuongeza umri wa wategemezi kutoka miaka 18 hadi miaka 21, kupandishwa vyeo vya watumishi, kubadilisha kada, kulipa malimbikizo ya watumishi pamoja na kutoa ajira mpya. 

About the author

mzalendoeditor