Mratibu wa ujenzi wa nyumba 3,500 Nzugani Dodoma (Awamu ya kwanza nyumba 150) Fedrick Jackson,akitoa maelezo kwa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa ziara ya kutembelea TBA na kujionea utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MUONEKANO wa nyumba 3,500 Nzugani Dodoma (Awamu ya kwanza nyumba 150)
KAMATI ya Baraza la wawakilishi inayohusiana na masuala ya Mawasiliano,ardhi na Nishati kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiendelea na ziara ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba awamu ya pili unaotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kuduma ya Baraza la Wawakilishi Kamati ya Mawasiliano,Ardhi na Nishati Mhe.Yahya Rashid Abdulla,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Miradi ya ujenzi wa nyumba 20 za viongozi, ujenzi wa nyumba 3500 wa nyumba za watumishi wa umma Nzuguni B na Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba awamu ya pili inayotekelezwa na Wakala wa majengo Tanzania (TBA ) jijini Dodoma.
MJUMBE wa Kamati ya Kuduma ya Baraza la Wawakilishi Kamati ya Mawasiliano,Ardhi na Nishati Mhe.Hussein Ibrahim Makungu akielezea ziara yao na kuipongeza TBA kwa kutekeleza miradi ya nyumba 3500 wa nyumba za watumishi wa umma Nzuguni B na Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba awamu ya pili inayotekelezwa na Wakala wa majengo Tanzania (TBA ) jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi,akizungumza mara baada ya Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea TBA na kujionea utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MKURUGENZI Idara ya Ushauri TBA Bw.Wencelaus Kizaba,akiipongeza Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo imetembelea TBA na kujionea utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba awamu ya pili inayotekelezwa na Wakala wa majengo Tanzania (TBA ) jijini Dodoma.
KAMATI ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea Miradi ya ujenzi wa nyumba 20 za viongozi, ujenzi wa nyumba 3500 wa nyumba za watumishi wa umma Nzuguni B na Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba awamu ya pili inayotekelezwa na Wakala wa majengo Tanzania (TBA ) jijini Dodoma.
…………………………………………….
Na Bolgas Odilo-DODOMA
KAMATI ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya Mawasiliano,Ardhi na Nishati imeridhishwa na jinsi Wakala wa Majengo nchini (TBA) unavyotekeleza miradi yake ambapo imesema imejifunza mambo mengi ambayo watashauri kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema mambo watakayoshauri ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kabla ya miradi pamoja na usimamizi wa sera,sheria na kanuni katika kutekeleza miradi mbalimbali.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Yahya Rashid Abdulla,mara baada ya kutembelea miradi mitatu ambayo ni ule wa Mji wa Kiserikali Mtumba awamu ya pili,ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma Nzuguni na mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi katika eneo la Kisasa .
Mhe.Abdulla ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza miradi hiyo mikubwa ambapo amesema hiyo ni hatua kubwa na wataenda kushauri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jinsi ya kutekeleza miradi.
“Ni wajibu wetu kuishauri Taasisi husika, nichukue nafasi hii kuipongeza Seriakali ya Jamhuri ya Muungano kwa kutekeleza miradi hii mitatu hii ni hatua kubwa na ni uwekezaji mkubwa sana utayari huu ni funzo kubwa ambalo tumelipata.
“Miundombinu hapa tayari kabla hata ya miradi hilo ni funzo pamoja na sera sheria na kanuni ili tuweze kupata ufanisi katika miradi yetu,”amsema.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati hiyo,ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtoni, Hussein Ibrahim Makungu ameshukuru kwa mashirikiano ambayo wamekuwa nao katika mambo ya maendeleo na wameona maendeleo ni makubwa hasa katika nyumba za viongozi na watumishi.
“Na mimi niseme katika kuona kwangu kote nimeona ufanyaji wa kazi niwapongeze sana TBA mpaka nimeuliza kuna Wakandarasi kutoka nje lakini nimeambiwa ni wa ndani niwapongeze sana.
“Tunataka kujifunza hata kuchukua wakandarasi kutoka Tanzania Bara waje watusaidie, kuliko kutoa nje tumeona matatizo mengi hili jambo ni zuri na tutaenda kuwaambia kule vijana wanasoma baada ya muda watakuwa wamemaliza,”amesema.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi amesema wamekuja kujifunza miradi hiyo kwa kutambua kwamba wanaingia katika kipindi cha bajeti.
“Ujio wetu ni kuona Serikali ya Tanzania inaendesha vipi miradi yake ,hii miradi yote ndio ndoto na kwetu Zanzibar kuja hapa ni kupata uelewa zaidi.Tumejifunza mambo mengi najionea maendeleo makubwa na mikakati ambayo imewekwa,”amesema.
Awali Mkurugenzi wa Huduma za Ushauri TBA,Wencelaus Kizaba amesema kwa awamu ya kwanza na pili katika mradi wa Mji wa Serikali Mtumba zimetengwa zaidi ya shilingi bilioni 620 kukamilisha miradi hiyo.
“Na kwa sisi TBA miradi ambayo tunaisimamia tumeweka timu ya wataalamu 50 ambao wanafanya kazi kila siku kuangalia changamoto zote ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.Kwa miradi mingine ni utoaji wa fedha kwa wakati tunaishukuru Serikali katika miradi yetu ile fedha imetoka kwa wakati,”amesema.
Aidha,ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea miradi hiyo ambapo amedai anaamini mashirikiano hayo yanataendelea ili na Zanzibar iweze kujenga miradi yenye viwango.
“Kwa kawaida mimi napenda kuishukuru Kamati ya Mawasiliano,Ardhi na Nishati kwa kuja kujifunza TBA inafanya kazi kwa namna gani na tumewatembeza.Tumeona wameshukuru na tunapenda ushirikiano uendelee na Zanzibar tumekuwa na mashirikiano kwa karibu na tuna miradi tunaifanya kule,”amesema.