NA
MWANDISHI WETU, DODOMA
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepewa Tuzo ya Kutoa Huduma
Rafiki kwa Wazee na Wagonjwa wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya
Mahali pa Kazi Duniani iliyofikia kilele leo Aprili 28, 2022 kwenye viwanja vya
Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Aliyekabidhi
Tuzo hiyo ni Mgeni Rasmi katika sherehe hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
na ilipokelewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, PSSSF, Paul Kijazi.
Siku
ya usalama na afya mahali pa kazi Duniani ni siku ya Kimataifa ya kufanya
kampeni ya kuboresha usalama na afya ya wafanyakazi, lengo ni kuondoa hali zote hatarishi mahali
pa kazi na hivyo kuifanya kazi iwe ya hadhi na heshima na hufanyika kila mwaka
kuelekea Siku ya Wafanyakazi Duniani yaani Mei Mosi.
Kwa
mujibu wa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Abdul Njaidi alisema ushiriki wa Mfuko
kwenye maonesho hayo ilikuwa ni fursa nzuri
ya kukutana na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla ambao walifaidika kwa
kupata elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mfuko.
Alisema
wote waliofika kwenye banda la PSSSF walikutana na wahudumu wa Mfuko ambao kazi
yao kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapokea wageni kwa bashasha na kutoa elimu
kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko, namna ya kupata taarifa za michango kwa njia
ya mtandao, jinsi ya mwanachama kuhakiki taarifa zake
“Majukumu
ya msingi ya Mfuko ni pamoja na Kuandikisha Wanachama, Kukusanya Michango,
Kulipa Mafao lakini pia Kuwekeza kwa njia ya hisa kwenye mabenki na kwenye
maeneo mengine kwa mujibu wa sharia” alisema na kuongeza……….Safari hii tumeshirikiana
na Kampuni yetu tanzu ya Kilimanjaro International Leather Industries Co.
Limited (KLICL) inayojisughulisha na
utengenezaji wa bidhaa za ngozi kama vile viatu, mikanda na mapochi.
Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (wapili kushoto),
akimkabidhi tuzo ya Kutoa Huduma Rafiki kwa Wazee na Wagonjwa wakati wa
Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi, Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw.
Paul Kijazi wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi
Duniani iliyofikia kilele leo Aprili 28, 2022 kwenye viwanja vya Kituo cha
Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma.