Featured Kitaifa

KINANA AWATAKA WABUNGE NA MADIWANI KUTOPITISHA SHERIA ZINAZOMINYA HAKI NA KUWABANA WANANCHI.

Written by mzalendoeditor

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wana CCM wa mkoa wa Tanga akiwa katika ziara ya kujitambulisha mara baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa Chama hicho.

…………………………………

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka madiwani na wabunge kukataa kupitisha miswada ya Sheria yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.

Pia, amesema Sasa ni wakati muafaka kulitazama vyema kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.

Kinana ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.

“Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue.

“Wabunge wa Bungee la Jamhuri ya Muungano…sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane na wananchi,” alisema.

About the author

mzalendoeditor