Featured Kitaifa

CHONGOLO: ‘WATU WA BAJAJI NA BODABODA HAWAWEZI KUONDOLEWA NI WATU MUHIMU”

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akihutubia Wajumbe wa Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Arnatoglo, Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.

SEHEMU ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar Es Salaam walioshiriki Kikao cha Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Wilaya ya Ilala ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Arnatoglo, Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.

SEHEMU ya Wajumbe waliohudhuria Kikao cha Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Wilaya ya Ilala ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Arnatoglo, Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.(Picha na CCM Makao Makuu)

……………………………………..

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema kuwa waendesha bajaji na bodaboda jji la  Dar es Salaam hawawezi kuondolewa katikati ya jiji hilo.

Chongolo ameyasema hayo, leo tarehe 22 Aprili, 2022 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilala.
 

Amesema kuwa, hao ni watu muhimu hawawezi kuachwa kwa sababu wanajitafutia riziki halali, ambapo amewasihi watu waache kutoa taarifa za kupotosha umma kuwa wanaondoshwa mjini.

“Kinachofanyika sio kuwazuia bodaboda na Bajaji wasiingie mjini bali ni kuwaratibu ili kuwawekea vituo rasmi zitavyoweza kutambulisha watu wanaohitaji kutumia usafiri huu”, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amesisitiza

Chongolo amesisitiza kuwa waendesha bajaji baadhi yao ni watu wenye ulemavu, ambao ni kundi maalum linalopata mikopo inayotolewa na Halmashauri asilimia 10, hivyo lazima waheshimiwe kwa kuwaweka eneo maalum kwa ajili yao ili wasigombanie abiria na watu wengine wasiokuwa na ulemavu.

Katika hatua nyingine, Chongolo amewakumbusha wajumbe wa kamati za siasa za ngazi zote wakiwemo viongozi wa Jumuiya ambapo kwa sasa kwa tathimini iliyopo Kamati hizo hazitekelezi majukimu sawasawa hasa kusimamia ajenda za wananchi.

About the author

mzalendoeditor