WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania uliofanyika leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania,Dk.Agnes Kijazi ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,akitoa taarifa wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania; Dkt. Buruhani Nyenzi,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Bi.Mariam Makomba,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
Meneja utawala na Rasilimali Watu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bi.Mariam Is-Haaq, akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma.
……………………
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa ihakikishe inakusanya mapato kwenye maeneo yote yaliyoainishwa na Sheria na yanazitumia huduma za hali ya hewa kibiashara.
Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 21,2022,Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.
Waziri Mbarawa amesema Wizara yake iko tayari kuwasaidia endapo kutatokea changamoto yoyote katika utekelezaji wa jukumu hilo la ukusanyaji wa mapato.
“Hata hivyo, kuna jambo ambalo nadhani ni vizuri mkalifamu na kulifanyia kazi.Majadiliano yenu yajikite kuwaelimisha wadau kuitekeleza Sheria.Kuchangia huduma ni suala la kisheria hivyo kila mdau hana budi kulitekeleza,”amesema.
Aidha,Prof.Mbarawa ameitaka Mamlaka hiyo iainishe bajeti na njia za ukusanyaji wa mapato ili kuiwezesha taasisi kujiendesha kwa ufanisi.
“Natambua Serikali ni mdau mkubwa katika huduma zitolewazo kwa jamii (Public Good), wakati Serikali inatekeleza jukumu hilo wadau wanaotumia huduma kibiashara nao pia watekeleze wajibu wao wa kuchangia huduma,”amesema.
Kuhusu changamoto ya maslahi duni,Prof. Mbarawa amesema Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – UTUMISHI inalishughulikia suala hilo ambapo ameahidi taratibu zikikamilika maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara itaboreshwa.
Pia, amesema amefurahi kusikia kuwa wapo katika hatua mbali mbali za majadiliano ya kukubaliana Tozo mpya kwa sekta nyingine.
“Mmetoa mfano wa sekta ya Ujenzi, Kwenye maji kwa maana ya wale wanao miliki vyombo, na watalii; ambao hawajaanza kuchangia, na kwamba majadiliano yanaendelea vizuri. Nawapongeza sana katika jitihada hizi,”amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania,Dk.Agnes Kijazi ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo amesema kuwa lengo la baraza hilo ni kupitia bajeti ya Mamlaka ya mwaka 2022/2023 na kufanya tathmini ya utendaji wa Mamlaka. Hii itasaidia kuongeza ubora na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma kwa lengo la kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
Dk.Kijazi amsema kuwa Mamlaka imehakikisha viwango na taratibu za kimataifa za utoaji wa huduma za hali ya hewa pamoja na usimikaji wa vifaa na mitambo vinazingatiwa.
“Kuidhinishwa kwa Muundo wa Taasisi na Miundo ya Maendeleo ya Watumishi (Schemes of Services). Muundo wa Mishahara bado unaendelea kufanyiwa kazi,”amesema
Pia,kuendelea na taratibu za ununuzi wa Rada nne za hali ya hewa zitakazofungwa katika Mikoa ya Mbeya, Kigoma, Dodoma na Kilimanjaro.
“Malipo ya awali yameshafanyika na Rada hizo zinaendelea kutengenezwa huko Marekani.Rada hizo zinatarajiwa kufungwa kati ya mwezi wa Julai, 2022 na Juni, 2023,”amesema.
Amesema TMA inakabiliana na changamoto ya maslahi madogo ya watumishi hali inayopelekea wataalamu kuhamia katika Taasisi zingine.