Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AJUMUIKA WANANCHI WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA KATIKA FUTARI MAALUM.

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja (hawapo pichani) katika futari maalum aliowaandalia katika ukumbi wa Michezani Mall Zanzibar jana 18-4-2022, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Shria Katiba, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kaabi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdalla Juma Mabodi.(

WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi katika futari maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Zanzibar.

WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) katika futari Maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Husseinn Ali Mwinyi katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Zanzibar jana 18-4-2022.

WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Michezani Mall Zanzibar.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwake) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Bi.Hamida Mussa Khamis, wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi.(hayupo pichani) baada ya kumazilika kwa hafla ya futari maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa Wananchi wa Mkoani wa Mjini Magharibi Unguja iliyofanyika katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Zanzibar j

Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor