KAMPUNI ya Huawei imetiliana saini makubaliano(MoU) na Chama cha Wadhibiti wa Mawasilinao Kusini mwa Afrika (CRASA) wenye lengo la kuongeza kasi mabadiliko ya kidigitali barani Afrika.
Makubalinao hayo yalitiwa saini na Katibu Mtendaji wa CRASA, Bi. Bridget Linzie na Mkurugenzi wa TEHAMA Idara ya Mikakati na Sera ya Huawei, Bw, Yang Hongjie, tarehe 29 Machi 2022 wakati wa Mkutano wa mwaka wa 11 wa CRASA uliofanyika Luanda nchini Angola na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 13 wanachama.
Chini ya makubaliano, pande zote mbili zinakusudia kubadilishana taarifa na mawazo juu ya sera na kanuni za TEHAMA, kufanya utafiti wa pamoja juu ya
usalama wa mtandao, ulinzi wa data, sera za jumuishi za kidijitali na teknolojia zinazoibukia kama vile 5G, na kuandaa shughuli za kujenga uwezo kupitia mikutano, warsha na mafunzo.
“Ninashukuru juhudi ambazo Huawei imekuwa ikichukua katika kuleta teknolojia za TEHAMA zenye ubunifu zaidi katika nchi za SADC kwa miaka kaadha sasa na kushirikisha uzoefu na ujuzi wake wa kimataifa katika ukanda huu. Tutafanya hivyo kuimarisha ushirikiano na Huawei ili kuharakisha zaidi mabadiliko ya kidijitali kwa ukuaji jumuishi katika kanda,” alisema Bi Bridget Linzie.
Mabadiliko ya kidijitali barani Afrika yalikua zaidi wakati wa janga la Uviko-19 na inatarajiwa kuendelea kukua katika kipindi cha baada ya janga, huku miundombinu ya TEHAMA na huduma zikizidi kuwa muhimu kwa ukuaji wa tasnia na maisha watu binafsi.
“Nina furaha kwamba CRASA itakuwa na Huawei kama mshirika wa kimkakati wa kuunda mustakabali wa TEHAMA katika ukanda huu kwa kutoa msaada katika kuunganisha nchi zisizounganishwa kidigitali.
Katika enzi hizi za uchumi wa kidijitali, ni muhimu sana kuweka mazingira yanayowezesha kutumia teknolojia mpya kama 5G kuendesha uchumi wa kijamii, kuendeleza na kuimarisha usalama wa mtandao na ulinzi wa data. CRASA inatazamia kwa ushirikiano mzuri na Huawei katika maeneo haya ya kitaalam,” alisema Bw. Alfred Marisa, akimwakilisha mwenyekiti wa CRASA.
“Huawei ina furaha kuwa na fursa ya kushirikiana na CRASA ili kuharakisha maendeleo ya TEHAMA katika ukanda. Tumekuwa tukifanya kazi na wadau muhimu katika sekta ya kujenga mfumo ikolojia mzuri ili kutimiza maono yetu ya kuleta dijitali kwa kila mtu, nyumba na shirika ili kujenga ulimwengu bora uliounganishwa na wenye akili,” alisema
Bw. Yang Chen, Makamu wa Rais wa Huawei Kanda ya Kusini mwa Afrika.
“Tunaamini hivyo na juhudi zetu za pamoja kati ya Huawei na CRASA, watu wengi zaidi wataweza kunufaika kutokana na ukuaji unaochochewa na maendeleo ya TEHAMA.”
Tangu iingie Afrika mwaka wa 1998, Huawei imekuwa ikishirikiana na waendeshaji wa ndani na washirika katika kutoa suluhu na huduma za kibunifu za TEHAMA kwa watu bilioni 1.1.