Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambapo itaanza kutumika baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Nembo ya vyeti maalum kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Sensa, kuashiria kumpa Jukumu la kuanza kazi hiyo rasmi wakati wa uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika, baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua rasmi Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika rasmi, baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SC Johnson ya nchini Marekani Bw. Fisk Johnson Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SC Johnson ya nchini Marekani Bw. Fisk Johnson na Ujumbe wake baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipofutarisha Viongozi na Wananchi mbalimbali wa Zanzibar Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar Jana tarehe 07 Aprili 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi na Wananchi mbalimbali wa Zanzibar baada ya futari aliyoiandaa Jana tarehe 07 Aprili 2022 Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi baada ya futari aliyoiandaa Jana tarehe 07 Aprili 2022 Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Nembo ya vyeti maalum kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu, kuashiria kumpa Jukumu la kuanza kazi hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambapo Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt. Hessein Ali Mwinyi.
………………………………………………………………..
RAIS SAMIA ATOA WITO KWA WANANCHI KUSHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza viongozi kutoa elimu na mafunzo kwa wananchi wote ili wajitokeze na kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akizindua Nembo na tarehe ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 katika Hoteli ya Golden Tulip.
Aidha, Rais Samia ameeleza kuwa ili Sensa ifanikiwe, uelimishaji na uhamasishaji ni masuala yanayotakiwa kupewa kipaumbele kuwasaidia wananchi kutoa taarifa kwa ajili ya kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha kupanga mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Rais Samia pia, amesisitiza elimu hiyo kutokana na changamoto za baadhi ya mila, desturi na imani potofu kwa baadhi ya jamii ambazo zinachukulia kuhesabiwa au kutaja idadi ya watoto au wanakaya waliopo ni kukaribisha laana na mkosi.
Vile vile, Rais Samia ameeleza mwenendo wa baadhi ya jamii au familia kuwaficha na kuwazuia watu wenye ulemavu kutoshiriki katika kuhesabiwa ni kinyume na haki za binadamu.
Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa taasisi za Serikali na taasisi binafsi kutumia Nembo ya Sensa katika shughuli zote za kiserikali na za sekta binafsi ili kuitangaza Sensa hadi itakapokamilika.
Tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanzania, tayari zimefanyika Sensa nyingine tano katika miaka ya 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.