Eintracht Frankfurt jana wamelazimishwa sare ya 1-1 na Barcelona katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya UEFA Europa League Uwanja wa Deutsche Bank Park Jijini Frankfurt, Ujerumani.
Frankfurt walitangulia kwa bao la Ansgar Knauff dakika ya 48, kabla ya Ferran Torres kuisawazishia Barca dakika ya 66.
Timu hizo mbili zilizoangukia kwenye michuano hiyo kutoka Ligi ya Mabingwa, zitarudiana Aprili 14 Hispania na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya West Ham United ya England na Lyon ya Ufaransa.