ABIRIA zaidi ya 50 waliokua wakisafiri kwa basi la Kampuni la Kampuni ya Skyline linalofanya Safari zake za Dar na Katesh Wilayani Hanang mkooani Manyara wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuteketea Kwa Moto likiwa njiani Katika Eneo Mtumbatu Wilayani Kilosa mpakani kabisa na Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Mashuda wa ajali hiyo walisema waliona Moto mkubwa chini ya Gari hilo na kianza kupiga kelele kwa dereva ambapo abiria waliokua ndani ya gari waliposikia kelele hizo ndipo nao walipopaza Sauti na ndipo dereva wa basi aliposimamisha.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Ahaji Majid Mwanga aliyefika katika eneo la ajali akifuatana na Katibu wa CCM Wilaya ya Kilosa Shaaban Mdoe pamoja na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama na kuzungumza na abiria hao alisema anachoshukuru ni kwamba hakuna madhara makubwa yaliyotokana na ajali hiyo ikiwemo majeruhi wala Vigo.
DC Mwanga aliwatoa hofu abiria hao kwani ulinzi na usalama wao pamoja na Mali zilizosalia utakuwepo wakati wote hadi pale usafiri wa kuwachukua na kuwafikisha mwisho wa safari yao utakapofika.
Pia Aliwaeleza abiria hao kuwa kuhusu upotevu wa mali zao mbalimbali utaratibu wa utambuzi na tathimini utafanyika kwa mujibu wa taratibu hivyo watoe shaka juu ya Mali zao Kwani basi hilo lina bima kwa mujibu wa taratibu za usafirishaji wa abiria.
Kw upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Kilosa amewataka madereva pamoja na wamiliki wa magari ya kusafilisha abili wa mikoani kukagua Magali Yao kabla ya kuanza safari Ili kuepusha ajali zinazosabaisha kwa Watanzania na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Mwisho.