Featured Michezo

MORRISON, KAGERE WAIPA POINTI 3 SIMBA

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna 

MABINGWA Watetezi Simba wameng’ara ugenini baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union  mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 39 likifungwa na Bernard Morrison baada ya beki wa Coastal kufanya uzembe ndani ya kumi na nane Morrison kuuwahi Mpira.

Kiungo Mkabaji kutoka Nigeria Victor Akpan aliisawazishia Coastal dakika ya 76 kwa shuti kali lililoenda moja kwa moja na kumuacha Aishi Manula.

Akitokea benchi Mshambuliaji hatari Meddie Kagere alipigilia msumari wa pili dakika ya 90+2 kwa bao safi huku Coastal walipata pigo dakika ya 87 kwa beki wake Patrick Kitenge kuonyesha kadi nyekundu. 

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 40 nafasi ya pili huku Coastal Union wakibaki nafasi ya 12 wakiwa na pointi 21.

About the author

mzalendoeditor