WAPINZANI wa Simba katika hatua ya Robo Fainali kujulikana kesho ambapo droo ya michezo ya hatua ya robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho itafanyika kesho Aprili 5, 2022 makao makuu ya CAF Cairo Misri.

Pia Droo hiiyo itahusisha jumla ya timu 8 kwenye kila michuan, zilizofuzu kutoka hatua ya makundi.

Simba pamoja na Pyramids, al- ittihad na Al Masry walimaliza katika nafasi za pili katika makundi yao na watakutana na timu hizi ambazo ni  Al-Ahli Sports Club ya Libya, TP Mazembe ya DR Congo, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na RS Berkane ya Morocco. 

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali upande wa klabu bingwa ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Raja Club Athletic ya Morocco, Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia na Wydad Athletic Club ya Morocco hizi zimemaliza kama vinara wa makundi.

Na zile zilizofuzu kama washindi wa pili kwenye makundi ni Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad, ES Setif zote za Algeria na Petro de Luanda ya Angola.

Timu zilizomaliza kama vinara wa Makundi zitapangwa juu halafu zilizomaliza nafasi ya pili zitachaguliwa kucheza na vinara wa makundi katika droo ya kesho. Lakini pia vinara hao wa makundi watapata faida ya kuanzaia ugenini kwenye michezo ya mkondo wa kwanza na mchezo wa pili watamaliza katika viwanja vyao vya nyumbani.

Katika hauta hii timu zilizokuwa kundi moja haziwezi kukutana lakini zile zinazotoka kwenye nchi moja zinaweza kupangwa kucheza kwenye hatua hii.

Previous articleWAZIRI VICKY FORD AZINDUA MPANGO WA ‘SHULE BORA’ KIBAHA
Next articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO APRIL 5,2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here