Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO KWA  MAAFISA UGANI AWATAKA KUTUMIA  VIFAA WALIVYOPEWA KWA KAZI ILIYOKUSUDIWA 

Written by mzalendoeditor

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akumuelezea kuhusu bidhaa mbalimbali za Kilimo kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia miche ya matunda ya miembe pamoja na michungwa katika mabanda ya Maonesho ya bidhaa za kilimo nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akizungumza wakati wa uzinduzi na ugawaji wa  vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika leo April 4,2022 Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ,akizungumza wakati wa uzinduzi na ugawaji wa  vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika leo April 4,2022 Jijini Dodoma.

SEHEMU ya Maafisa Ugani wa Kilimo wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbalimbali ya zao la mpunga ambao umekobolewa katika viwango mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu na utengenezaji wa nafaka kwa ajili ya mifungo katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele uliowekwa kwenye kifungashio kwa ajili ya kupelekwa sokoni katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Taifa Jacqueline Mkindi kuhusu zao jipya la kilimo pamoja na mazao mbalimbali ya Biashara katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu zao la parachichi ambalo limekuwa likiwaletea tija wakulima nchini hususan katika Mikoa ya Njombe, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya ukaguzi wa mabanda mbalimbali ya wakulima pamoja na Wafanyabiashara leo tarehe 04 Aprili, 2022 Jijini Dodoma.

Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi na ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akigawa pikipiki kwa waakilishi wa Maafisa Ugani 7000 katika hafla iliyofanyika nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04, Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akielezea kuhusu vitendea kazi kwa Maafisa Ugani Kilimo kabla ya uzinduzi katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Pikipiki Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwasha Pikipiki mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

…………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka maafisa ugani wa kilimo nchini kutumia vifaa hivyo kwa makusudu yaliyo kusudiwa ili kuleta tija katika sekta ya kilimo.
Rais Samia amebainisha hayo leo April 4,2022 jijini Dodoma wakati akizindua  vitendea kazi vya maafisa ugani wa kilimo nchini ambapo amesema pamoja na kutoa vifaa hivyo atawapima utendaji wao ili kuleta tija katika sekta ya kilimo
Mhe. Samia amesema kuwa sekta ya kilimo imeendelea kuwa muhimili Mkuu wa kukuza uchumi nchini na kuleta maendeleo ndani ya nchi
“Serikali inaendelea kuimarisha huduma za ugani kwa kugawa pikipiki 6700 leo na pikipiki 300 zilishagawa hapo kabla na kufanya jumla ya pikipiki zilizogawiwa kuwa 7000”, ameeleza Rais samia
Rais Samia amesema kuwa Serikali imeweza kufanikisha kupatikana kwa udhibiti ubora wenye viwango vya kimataifa kwa maabara zetu za mimea  viuatilifu
“Tumefanikiwa kugawa masoko ya mazao mbalimbali ikiwemo zao la parachichi katika nchi za India na Afrika kusini na hii ni baada ya kukidhi viwango vya ubora
Kwa mwaka wa 2020 sekta ya kilimo imekuwa kwa asilia 4 .9 na kuchangia asilimia 26 katika pato la taifa
Rais Samia amesisitiza kuwa kama nchi kuna kazi kubwa ya kufanya kilimo cha umwagiliaji maji na kilimo cha kisasa ili kufikia malengo yaliyopangwa na serikali.

Pia miongoni mwa Malengo Matano ya serikali katika kuongeza kasi ya kilimo ,kuongeza thamani ya mazao tunayouza nje, kuongeza idadi ya mashamba makubwa kutoka 110 hadi 1000, kuongeza umwagiliaji kutoka asilimia 10 hadi asilimia 50.
Sekta ya kilimo imetoa ajira kwa asilimia 61 ya watu wote na pia asilimia 65 ya malighafi lakini pia ni sekta inayofanya tujitosheleze kwa chakula.
Aidha Rais Samia Rais samia amesema kuwa kiwanda cha tumbaku mjini Morogoro kinakwenda kufunguliwa na hilo linatokana na uzalishaji wa tumbaku kuongezeka.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezipongeza taasisi za fedha kwa kuwapatia mitaji wakulima kwa viwango vya kuridhisha ambapo kila mkulima anaweza kumudu

‘Nalipongeza bunge kupitia kamati ya kilimo, mifugo na maji kwa kazi nzuri ya kushauri na kuisimamia serikali kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi lakini pia kupitisha bajeti kwaajili  ya utekelezaji wa miradi yote ya kilimo.’amesema Mhe Majaliwa

Naye  Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Rais Samia  kumpatia Sh150 bilioni ili aziweke katika benki za biashara kama dhamana (security), hatua itakayowezesha wakulima nchini kuanza kupata ruzuku ya mbolea katika msimu wa kilimo ujao.

Amesema Rais Samia aliielekeza Benki Kuu (BoT) kutenga Sh1 trilioni kwa ajili ya sekta ya kilimo na kumuomba Sh150 bilioni kwa ajili ya kuweka katika benki za biashara kama security.

Amesema hatua hiyo itawezesha kuaanza kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu ujao wa kilimo.

Aidha Bashe alisema,licha ya mipango na mikakati mingi iliyopo lakini kumekuwa na changamoto kubwa ya pembejeo huku akisema kwa uoande wa mbolea katika soko la Dunia kwa sasa imepanda kwa zaidi ya asilimia 300.

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa ofisi yake wamefanya vikao na wataalam wao na watatekeleza maagizo yote kutoka kwa wizara ya kilimo na hakutakuwa na visingizio baada ya kuwapatia vitendea kazi kupatikana.

Awali  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa waliweka nguvu kubwa katika kilimo Cha Alizeti ambapo Kwa takwimu zilizopo wameweza kufanya vizuri.

“Sisi kama Dodoma tulikubaliana kuweka nguvu kwenye kilimo Cha Alizeti na tumefanya vizuri tunashirikisha watu wa mabenki ili kufanya kilimo chenye tija tumshukukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi Dodoma”amesma Mtaka

About the author

mzalendoeditor