Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka baada ya kuwasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 3 – 5 Aprili 2022.
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masshariki Balozi Fatma Rajab baada ya kuwasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 3 – 5 Aprili 2022.
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford akizungumza na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Dodoma baada ya kuwasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 3 – 5 Aprili 2022.
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford akisaini kitabu cha wageni katika uwanja wa ndege wa Dodoma baada ya kuwasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 3 – 5 Aprili 2022.
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford (katikati) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concor akifuatilia mazungumzo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford (katikati) huku Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concor (kulia) akifuatilia mazungumzo hayo
…………………………………………………………
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford amewasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 3 – 5 Aprili 2022.
Waziri huyo amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab.
Baada ya kuwasili jijini Dodoma Waziri Ford alielekea Ikulu ya Chamwino ambako alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznsia Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.
Katika ziara yake nchini Mhe. Ford pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kuzindua mpango mpya wa Elimu bunifu nchini ambao unafadhiliwa na serikali ya Uingereza.
katika ziara yake nchni Waziri Ford ataungana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa kuzindua mpango huo mpya wa maendeleo wa elimu bunifu nchini unaoitwa Shule Bora utakaofanyika Kibaha mkoani Pwani tarehe 04 Aprili 2022.
Mpango wa Shule Bora utaongeza upatikanaji wa elimu kwa watoto zaidi ya milioni nne (4) nchini, umelenga kuboresha viwango vya elimu kwa watoto wenye ulemavu, watoto wanaotoka maeneo yenye upungufu wa rasilimali na wasichana.
Kati ya mwaka 2015-2020 Uingereza kupitia ufadhili katika sekta ya elimu imesaidia zaidi ya watoto milioni 15.6 duniani kote kupata elimu, ikiwa ni pamoja na wasichana milioni 8.1.
Waziri Ford pia atakuwa na mikutano na ziara mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kazi mbalimbali zinazofanywa nchini katika kuimarisha uhusiano kati ya Uingereza na Tanzania kupitia nyanja za biashara, mabadiliko ya tabianchi na kupambana na uhalifu mkubwa na uliopangwa.