Featured Kimataifa

RUTO AMUOMBA RADHI RAILA ODINGA

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais nchini Kenya William Ruto amemuomba radhi Kiongozi wa Chama cha ODM na Mgombea wa kiti cha Urais Raila Odinga kufuatia shambulio lililofanywa kwa msafara wake juzi tarehe Mosi Aprili.

Ruto amemtaka Inspekta Generali wa Polisi Hillary Mutyambi kuwakamata vijana walioharibu helikopta na magari katika msafara huo.

Ruto amesema kuwa kilichotokea kwa Odinga katika kaunti ya Uasin Gishu ni kitu cha kujutia.

About the author

mzalendoeditor