Featured Kimataifa

‘NUSU YA MIMBA DUNIANI HAZIKUTARAJIWA’:UNFPA

Written by mzalendoeditor

Ripoti ya Hali ya ldadi ya Watu Duniani mwaka 2022, iliyotolewa Machi 30, 2022 na Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulika na Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA) imeonesha kuwa karibu nusu ya mimba zote ambazo ni jumla ya milioni 121 kila mwaka Duniani kote, hazikutarajiwa

Ripoti hiyo imeonesha waathirika wakubwa ni wanawake na wasichana, kwani wanakuwa hawana maamuzi yao kama wanataka kuwa wajawazito au la licha ya kuwa wao ndiyo wanaobeba ujauzito

Asilimia 60 ya mimba hizo zinatolewa huku asilimia 45 ya mimba zinazotolewa, hazitolewi katika njia salama na kusababisha vifo kwa asilimia 5 hadi 13

About the author

mzalendoeditor