Featured Michezo

ALGERIA YAPELEKA BARUA YA RUFAA FIFA KISA CAMEROON

Written by mzalendoeditor

Shirikisho la soka nchini Algeria (FAF) limeomba kipindi cha pili cha mechi yao dhidi ya Cameroon kirudiwe.

Habari zinasema kuwa FAF imepeleka barua rasmi ya maombi na rufaa kwa FIFA kwa kile walichokiita ” maamuzi yenye kashfa yaliyopotosha matokeo”.

FAF imesema iko tayari kutumia njia zote zilizo halali kupata haki yao na mechi hiyo ambayo walitolewa kwa goli 2-1 kurudiwa tena.

About the author

mzalendoeditor