Featured Kitaifa

SILINDE ATAKA MAAFISA ELIMU KUSIMAMIA UPATIKANAJI WA TAARIFA SAHIHI ZA WANAFUNZI WALIOACHA SHULE

Written by mzalendoeditor

NAIBU  Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Mhe. David Silinde,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mafunzo Elekezi kwa Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri Tanzania bara uliofanyika leo Machi 31,2022 jijini Dodoma.

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Gerald Mweli,akitoa maelekezo kwa maafisa Elimu wakati wa Mkutano wa Mafunzo Elekezi kwa Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri Tanzania bara uliofanyika leo Machi 31,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Mhe. David Silinde (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mafunzo Elekezi kwa Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri Tanzania bara uliofanyika leo Machi 31,2022 jijini Dodoma.

Afisa Elimu ya Watu Wazima Bagamoyo Bi. Martha Ignatus,akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Mhe. David Silinde,mara baada ya kufungua Mkutano wa Mafunzo Elekezi kwa Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri Tanzania bara uliofanyika leo Machi 31,2022 jijini Dodoma.

………………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imewataka Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri kusimamia upatikani wa taarifa sahihi za wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali ili waweze kurudi shuleni.

Hayo yamesemwa leo Machi 31,2022 jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Mhe. David Silinde wakati akifungua Mkutano wa Mafunzo Elekezi kwa Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri Tanzania bara .

Mhe. Silinde amewataka wasimamizi wa elimu ya watu wazima kufanya kazi kwa weledi ili nafasi iliyotolewa na Serikali kwa wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali waweze kurudi shule kuendelea na masomo.

Aidha ameeeleza kuwa Serikali inatambua kuwa jamii iliyoelimika yenye maarifa, ujuzi na uzalendo ndio msingi wa maendeleo ya ujengaji wa uchumi hasa ujenzi wa uchumi wa viwanda.

“Haya ni sababu ya usimamizi mzuri wa elimu ya Awali, Msingi Sekondari na Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo rasmi” amesema Silinde

Hata hivyo Silinde amesema kuwa kuwepo kwa mpango wa uwiano kati ya elimu na jamii(MUKEJA) na Mpango wa elimu ya msingi kwa watoto walioikosa (MEMKWA).

‘Serikali inatambua umuhimu wa elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi kupitia Sera ya elimu ya mwaka 2014 tamko namba 3.3.3. hii ni kutoa nafasi kwa waliokosa fursa katika mfumo rasmi ili kujiendeleza na kutatua changamoto za maisha au kuhitimu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.’ameeleza

Silinde ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia ili kupata idadi kamili ya walengwa wa elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi.

‘Ninawaelekeza mkafatilie upatikanaji sahihi wa takwimu za elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi kwa kuendelea kuutumia mfumo wa BEMIS’

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Gerald Mweli amewataka kuendelea kusimamia na kufuatilia wanafunzi wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali.

Bw.Mweli amesema kuwa mpaka sasa takwimu zinaonesha zaidi ya wanafunzi 909 wamesharudi shule kuendelea na masomo kati ya hao wapo wenye sababu mbalimbali zikiwemo utoro na ujauzito.

“Nitoe wito hii idadi ya wanafunzi waliorudi darasani kazi kubwa nyie ndio mmeifanya na Serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan inatambua kazi yenu ndio mana imetoa fursa wanafunzi wote walioacha shule warudi darasani tekelezeni majukumu yenu tunajua bado wengine wapo tumieni taratibu za kazi zenu ili kusiwe na sababu ya mtu kukosa elimu kwa kukosa fursa ambayo Mhe. Rais ameitoa.’amesema Mweli

Hata hivyo  Silinde amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmshauri zote kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi na kuzisimamia utekelezaji wake.

Naye Afisa Elimu ya Watu Wazima Bagamoyo Bi. Martha Ignatus, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya watumishi na kuahidi maelekezo yote wanaenda kuyafanyia kazi na kuahidi upatikanaji sahihi wa takwimu.

About the author

mzalendoeditor