Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo kilichofanyika leo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasili Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo wakati wa wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo. Aliombatana nao ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni na Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye.
Mkurugenzi wa Intelijensia –TAKUKURU, Bw. Malimi Mifuko akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye kikao kazi chake na Menejimenti hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) baada ya kumaliza kikao kazi chake na Menejimenti hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) makao makuu jijini Dodoma mara baada ya kikao kazi chake na Menejimenti ya TAKUKURU.
……………………………………………………..
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameielekeza Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha wanayaishi maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mipango na huduma za maendeleo zinawafikia wananchi kwa ukamilifu.
Mhe. Jenista amesema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti ya TAKUKURU alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.
Mhe. Jenista amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali anayoiongoza ya Awamu ya Sita imejipanga kikamilifu kuleta mageuzi makubwa kwenye taifa katika sekta zote ili wananchi wapate huduma bora na kwa wakati, hivyo, TAKUKURU wanao wajibu wa kuhakikisha maono ya Mhe. Rais pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita yanafikiwa kwa ukamilifu.
“TAKUKURU tuna deni kubwa sana kwa Watanzania katika kuhakikisha mipango na huduma zinazotakiwa kuwafikia Watanzania zinawafikia kwa ukamilifu,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Ameongeza kuwa, yale ambayo Watanzania wanafikiria Serikali yao iwafanyie, hayawezi kufanikiwa kwa ufasaha kama miongoni kwa taasisi wezeshi ikiwemo TAKUKURU isipofanya kazi yake sawasawa.
“Ili taifa liweze kupiga hatua kimaendeleo, basi TAKUKURU katika kutekeleza majukumu yetu ni lazima tuzingatie Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo uliopo, maono ya Mhe. Rais aliyepo madarakani pamoja juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kufanya mabadiliko makubwa ya mwenendo mzima wa uchumi, upelekaji wa huduma kwa wananchi, nidhamu, maadili ya taifa hili,” Mhe. Jenista amefafanua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Hamduni amemshukuru Mhe. Waziri kwa kufanya nao kikao kazi na kuahidi yeye pamoja na watendaji wengine kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa ili kuendana na matarajio ya Serikali ya kufikisha huduma bora kwa umma.