Featured Kimataifa

WAKUU WA NCHI ZA EAC WAIPITISHA RASMI DRC CONGO KUWA MWANACHAMA KAMILI

Written by mzalendoeditor
Wakuu wa nchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao chao cha 19  kilichofanyika kwa njia ya mtandao.
Katikati ni katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Peter Mathuki akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya jumuiya hiyo mara baada ya kikao cha wakuu wa nchi wanachama kumalizika.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kikiwa kinaendelea kwa njia ya mtandao.
……………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki wameipitisha Jamuhuri ya Demokrasia vya  Congo(DRC) kuwa mwanachama  kamili wa jumuiya hiyo leo March 29, 2022 katika kikao chao cha 19 kilichofanyika kwa njia ya mtandao.

Kikao hicho kilichodhururiwa na Wakuu wa nchi ambao ni Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Samia Suluhu wa Tanzania, Rais Yoweri Museveni  wa Uganda, Rais Paul Kagame Rwanda, Makamu wa Rais wa Burundi Prosper Bazomba’nza, Waziri wa nchi ofisi ya Rais wa Sudan Kusini Dkt. Barnabas Benjamin pamoja na Rais wa Congo Felix Tshisekedi.
Katibu Mkuu wa wa jumuiya hiyo  Dkt. Peter Mathuki alisema kuwa ni siku kuu na heshima kwa jumuiya kwa wakuu wa nchi wanachama kuipitisha DRC kujiunga na EAC kwani kuna faida kubwa za kiuchumi, kisiasa na kiulinzi ndani  ya  jumuiya hiyo.
Dkt Mathuki alisema Katika nyanja ya kiuchumi, soko la jumuiya ya Afrika Mashariki, sasa linaongezeka kutoka milioni 190 na kuwa na watu zaidi ya milioni 250 na kufanya kuwa miongoni mwa jumuiya kubwa za kikanda zenye watu wengi .
Alisema  ni furaha yao na wananchi wa EAC kwani kupitia kujiunga kwa Congo DRC kutaongeza fursa za kiuchumi na kibiashara katika kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.
“Nchi hizi zikiondoa vikwazo mipakani katika kufanya biashara zitaongeza nafasi za ajira kwa wananchi kwani ndio lengo kuu wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya mashariki,”Alisema Dkt Mathuki

About the author

mzalendoeditor