Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 akishiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa North Hall kushiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
…………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo ambapo
Pamoja na mambo mengine lina lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana mbinu za kuimarisha utendaji wa serikali.
Katika Ufunguzi wa Jukwaa hilo viongozi wakuu wa serikali, mashirika ya kimataifa pamoja na sekta binafsi kutoka nchi mbalimbali wamekutana na kujadili namna bora ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za serikali kwa wananchi na kutatua changamoto mbalimbali kupitia utafiti kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea duniani.
Hapo kesho tarehe 30 Machi 2022 Makamu wa Rais Dkt. Mpango anatarajiwa kuzungumza katika jukwaa hilo akichangia mada ya “kwanini Afrika imekua ni muhimu sana kwa wakati huu katika uchumi wa dunia”