Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mohamedi Bakari Lukindo, mwenye umri miaka 43 kwa tuhuma za kumuua Athumani Dolly baada ya kumfumania na mke wake, nyumbani kwake mtaa wa Vunja Bei wilayani Handeni.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Safia Jongo ameeleza kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Machi 28, 2022 baada ya Mohammed kumkuta mkewe Rehema Barau akiwa na Athumani ndani nyumba yao ambapo alianza kumshambulia.

Kamanda Jongo amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa wa mauaji Mohammedi kumshambulia Athumani hadi kufa.

 Ameongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua undani wake, muhusika aliyefanya tukio hilo ameshakamatwa.

“jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na tutatoa taarifa zaidi,” amesema Kamanda Jongo.

Previous articleUBORESHAJI WA KARAKANA WAZIDI KULETA TIJA TBA
Next articleTANZANIA YASHIRIKI MAKABIDHIANO YA MAJUKUMU YA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here