Featured Kitaifa

MBUNGE WA JIMBO LA ULANGA ATOA MABATI NA CHAKULA CHENYE THAMANI YA ZAIDI YA MIL 41 KWAAJILI YA WAHANGA WALIOEZULIWA NYUMBA ZAO NA UPEPO

Written by mzalendoeditor

MBUNGE
wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe  Salim Alaudin Hasham wa pili
kutoka kushoto akikabidhi msaada kwa unga kwa baadhi ya wahanga hao
ambapo ametoa bati
1190 mifuko ya Sembe 321 na Mbao za kuezekea nyumba kwaajili ya Kaya
zilizoezuliwa nyumba zao na upepo mkali kuanzia mwezi wa kwanza 1 mpaka
mwezi wa tatu.

MBUNGE
wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe  Salim Alaudin Hasham aliyevaa
shati la draft akiwa na unga na mabati kabla ya kuvikabidhi kwa wahanga
ambapo ametoa bati
1190 mifuko ya Sembe 321 na Mbao za kuezekea nyumba kwaajili ya Kaya
zilizoezuliwa nyumba zao na upepo mkali kuanzia mwezi wa kwanza 1 mpaka
mwezi wa tatu.
MBUNGE
wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe  Salim Alaudin Hasham akizungumza wakati wa halfa hiyo

MBUNGE
wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe  Salim Alaudin Hasham ametoa bati
1190 mifuko ya Sembe 321 na Mbao za kuezekea nyumba kwaajili ya Kaya
zilizoezuliwa nyumba zao na upepo mkali kuanzia mwezi wa kwanza 1 mpaka
mwezi wa tatu.

Akizungumza
katika mkutano na wananchi wa Tarafa ya mwaya Mbunge Salim Alaudin Hashamamesema amefanya hivyo kwa lengo la kuhakikisha kila familia
inarejea kwenye mazingira ya awali waliyokuwa wanaishi ili waendeleze
maisha kama zamani na waendelee kujitafutia kipato.
Hali
hiyo inakuja baada ya ziara yake aliyoifanya wiki mbili zilizopita ya
kukagua nyumba zilizoezuliwa na upepo na kujionea namna wananchi
walivyopoteza makazi yao na vyakula kwa kipindi cha miezi mitatu.
Jumla
ya Kaya 321 zilipata maafa hayo ya kuezuliwa paa za nyumba zao lakini
mpaka sasa jumla ya Kaya 119 bado hazijarejea kwenye makazi yao kutokana
na kushindwa kumudu gharama za kurekebisha makazi hayo.
Mbunge
SALIM ametoa bati 10 kwa kila Kaya na mbao kwa Kaya 119 ambazo hazina
makazi mpaka sasa na pia ametoa mfuko mmoja wa sembe kwa kila Kaya kwa
jumla ya Kaya 321 ili kujikimu kwa chakula.
Aidha
Mbunge SALIM ALAUDIN HASHAM amesema pia fedha hizo alizotumia ni kutoka
mfukoni mwake na amefanya hivyo kwa lengo la kuona kila Mwananchi wa
jimbo lake anapata ahueni ya Machungu hayo.
Jumla
ya vijiji 15 vya wilaya ya Ulanga vilikumbwa na maafa ya kuezuliwa
mapaa ya nyumba za wananchi kuanzia mwezi wa kwanza mpaka tatu.

About the author

mzalendoeditor