WAZIRI
wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya Kufungua Tamasha la
Tanga Utalii Festival leo Jijini Tanga lililofanyika viwanja vya Urith
Jijini humo ambalo liliandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim
Mgandilwa
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa Tamasha hilo |
Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Calvas Joseph akizungumza wakati wa Tamasha hilo |
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo kutoka kwa Bandari ya Tanga mara baada ya kutembelea banda lao
WAZIRI wa Afya akipata maelekezo kwenye Banda la Benki ya Tanzania Comercial Benki wakati alipotembelea Banda lao
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza kutoka kwa Benki ya NMB wakati alipotembelea Banda lao
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kushoto akipata maelezo kwenda Banda la Magoroto |
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akipokea tisheti wakati wa tamasha hilo |
NA OSCAR
ASSENGA,TANGA
WAZIRI wa
Afya Ummy Mwalimu amefungua Tamasha la Tanga Utalii Festival huku akipigia chapuo vivutio vya utalii vilivyopo Jijini Tanga kwa
kuwashauri watalii wanapokwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
waunganishe na Tanga kuona vuvutio vingine ikiwemo Beach nzuri,Visiwa vya Toten
na Mapango ya Amboni.
Amesema pia Tamasha
hilo la Tanga Utalii Festival litafungua fursa na kuongeza za kipato kwa wananchi
wa mkoa wa Tanga na hivyo kuchochoe ukuaji wa uchumi kwa mkoa huo.
Ummy
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) aliyasema hayo leo wakati
akifungua Tamasha la Tanga Utalii Festival ambalo limefanyika
kwa mara ya kwanza ambalo limeandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim
Mgandilwa na kushirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali.
Alisema upo
umuhimu wa watalii wanapokwenda kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
wanapomaliza badala ya kurudi uwanja wa ndege Kia watumia fursa hiyo kuja
mkoani Tanga ili kuweza kuona vivutio adimi vilivyopo ikiwemo beach,visiwa na
eneo la magoroto lenye vipepeo ambavyo havipatikani mahali pengine popote
duniani.
Waziri Ummy
alisema kwamba wanaweza kutumia jukwaa hilo ambalo kwa sasa litakuwa
likifanyika kila mwaka kuhakaikisha wakuza fursa za ajira na uchumi kwa watu wa
Tanga.
“Tunataka
kulifanya Jiji la Tanga kuwa la Mahaba watu wa Mwanga na Same wanapokuja
kutalii Mkomazi tuna maombi yetu watu wasiiishie mkomazi waje na Tanga
tuwapeleke visiwa vya toten,beach Usongo Pangani ambapo kuna mchanga mzuri
halafu waende Magoroto Muheza wanaona vipepeo”Alisema
Hata hivyo
alisema jambo hilo ni nzuri na wao wataendelea kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya
Tanga huku akieleza kwamba Rais Samia Suluhu ametoa Milioni 500 kwa Jiji la
Tanga kwa ajili ya kujenga Machinga Complex.
“Kwa kweli
nimpongeza Dc Mgandilwa kwa kuandaa Tanga Utalii Festival ni jambo nzuri lengo
lake ni kutaka kuonyesha utamaduni wa Tanga uzuri mila za Tanga nitoe wito kwa
wakazi wa Tanga na nje ya Tanga kutembelea vivutio vilivyopo katika mkoa wa
Tanga yakiwemo Mapango ya Amboni tunashukuru Mamlaka ya Ngorongoro
wanayaboresha kila siku”Alisema
“Lakini Tanga
pia tuna kisima cha maji Moto,Beach nzuri za kutembelea,kisiwa cha Toten
tunaposema tunataka kulifanya Jiji la Tanga kuwa la mahabaa ukarimu na maendeleo
ni kuonyesha mambo mazuri tulionayo ni jambo nzuri na sisi viongozi wenye asili
ya Tanga tutakuunga mkono kuhakikisha tunaliboresha kila mwaka”Alisema
Awali
akizungumza wakati wa tamasha hilo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema
waliona watumie jukwaa hilo kutangaza fursa za utalii uliopo Jijini Tanga
ikiwemo Visiwa,Mapango na Makaburi ya Shabani Robert kwani waliona bado
hayajatangaza ipasavyo.
Alisema
sambamba na kutangaza vivutio hivyo lakini pia kutangaza Utalii uliopo eneo la
Magoroto wilayani Muheza ikiwemo na baadhi ya samaki silikant huku akieleza
kuanzishwa kwa tamasha hilo ni kutangaza vivutio vilivyopo kwa wadau.
Mkuu huyo wa
wilaya alisema lengo lengine ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo na kuhamasisha
sensa ya watu na makazi kwa wananachi na wanaamini tamasha hili litakuwa
endelevu lengo ni kutangaza utalii .
Naye kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo alisema wamekuja kumuunga
mkono Waziri Ummy kutokana na kazi nzuri anayoifanya nchi na jimbo na wilaya ya
Same umekuja kufanya kazi kubwa na nzuri hivyo pia niwahamasisha wananchi kutembelea
vuvutio vya utalii vilivyopo nchini.
Hata hivyo
Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya Alisema wao kama wakuu wa wilaya za
mkoa wa Kilimanjaro wameona kuna umuhimu wa kuja kuunga mkono tamasha hilo.