Featured Kitaifa

MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA GEITA YANUNUA MASHINE 10 ZA FIGO

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule ameseka kuwa katika Kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Hassan akiwa madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoa wa Geita umepokea jumla ya Bilioni 54 kwa ajili ya miradi ya Sekta ya afya na miongoni mwa fedha hizo Bilioni 6 zimetumika kununulia vifaa tiba ikiwa ni pamoja na kununua Mashine 10 za kusafisha Figo katika Hospitali ya Kanda ya Ziwa iliyoko Wilayani Chato.

Senyamule amesema kuwa kwasasa Hospitali hiyo inafanya kazi kwa kutibu magonjwa ambayo siku za nyuma wagonjwa walikuwa wanalazimika kupewa rufaa kwenda kutibiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule amesema hayo leo Machi 24,2022 wakati akifungua Jukwaaa la Wanawake wa Mkoa wa Geita katika ukumbi wa Gedeco Mjini Geita.

Amesema kuwa katika Kipindi hicho cha mwaka mmoja wa Rais Samia Hassan mkoa wa Geita umepokea jumla ya Bilioni 188.9 ambazo zimeelekezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mkoa wa Geita umezindua rasmi jukwaa la Wanawake ikiwa ni miezi michache Rais Samia Hassan akiwa ameelekeza Mikoa yote kuanzisha majukwaa hayo na eye kuwa mlezi wa mabaraza hayo.

Chanzo:Mwangazatv

About the author

mzalendoeditor