Featured Kitaifa

WANAOTUMIA DAWA ZA KUONGEZA HAMU YA KUFANYA MAPENZI WAPO HATARINI KUPATA SARATANI

Written by mzalendoeditor

MTAALUMU wa Afya amewashauri Wanawake  wanaotumia dawa za kuongeza hamu ya kufanya tendo la ngono kuacha kutumia dawa hizo ambazo hazijapimwa na wataalamu katika sehemu zao za siri, kwa kuwa kufanya hivyo kunawaweka hatarini kupata Saratani ya Shingo ya Kizazi

Mtaalamu na Mshauri wa Afya ya Umma, Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Dkt. Katanta Simwanza amesema takwimu za mwaka 2021 za Saratani katika Hospitali ya Ocean Road zinaonesha aina ya Saratani zinayowapata Wanawake wengi ni Saratani ya Shingo ya Kizazi (43%), Saratani ya Matiti (14.2%) na Saratani ya Koo (3.8%)

Ametaja utumiaji wa dawa za kusisimua mwili ambazo hazijapimwa, ngono zisizo salama, kushiriki tendo la ndoa mapema, kujamiiana na wanaume wasiotahiriwa, matumizi ya virutubisho kama potasiamu ili kuongeza hamu ya ngono vinaweza kuwa chanzo, cha Saratani hizo na pia vinaweza kusababisha kuondolewa kwa harufu ya asili ukeni

About the author

mzalendoeditor