Featured Michezo

KASI YA YANGA HAISHIKIKI YAICHAPA KMC LIGI YA NBC

Written by mzalendoeditor

KASI ya Yanga haishikiki katika kutafuta  ubingwa wa  28 baada ya kuichapa  mabao 2_0 KMC mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. 

Yanga walipata bao mnamo dakika ya 38 baada ya Beki wa KMC Vicent Andrew akisindikiza Mpira wa Fiston Mayele.

Shabani Djuma aliipatia Yanga bao la pili dakika ya 52 akimalizia Mpira wa Kona iliyopigwa na Chico Ushindi.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 48 na kuendelea kushikilia usukani wa Ligi hiyo huku KMC wakibaki nafasi ya 7 kwa Pointi zao 22.

Kabla ya mechi kuanza kulikuwa na burudani kwa mechi kati ya Viongozi wa Yanga na Wasanii wa bongo fleva na bongo muvi na baadae kulipigwa burudani ya Muziki kama maadhimisho ya mwaka mmoja ya Rais Samia tangu aingiee madarakani na ulishuhudiwa na Rais Mstaafu Mhe.Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Rais Samia.

 

About the author

mzalendoeditor