Featured Kitaifa

BREAKING NEWS:AJALI YA BASI, YAUA WATU 13 MOROGORO,RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA POLE

Written by mzalendoeditor
************
WATU 13 wamefariki Dunia na wengine 32 kujeruhiwa baada ya basi lenye namba za usajili T 732 ATH mali ya Kampuni ya AHEED linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Tanga kugongana na lori lenye namba IT 2816.
Akizungumza Kwa njia ya simu na fullushangwe Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Futunatus Muslim amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Malela wilayani Mvomero mkoani hapa.
Amesema majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Samia Suluhu@SuluhuSamia

Nimesikitishwa na vifo vya watu 22 vilivyosababishwa na ajali ya basi kugongana na lori katika eneo la Melea Kibaoni, Morogoro. Nawapa pole wafiwa, nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka. Nawasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani.

IMG_20220318_205837

About the author

mzalendoeditor